Kama ni hivyo basi kwanini tumetafuta elimu ?!

سب رجل الإمام وكيع- رحمه الله- فلم يُجبه

Kuna mtu alimtukana imamu Waki’i -Allah amrahamu- lakini (yeye) hakumjibu (kitu)

فقيل له : ألا ترد عليه ؟

akaambiwa : Hivi kwanini humrudishii?

قال : و لم تعلمنا العلم إذاً

Akasema: kama ni hivyo (basi) kwanini tumetafuta elimu

📚- روضة العقلاء صـ١٦٦ –

Maelezo ya mfasiri:

Miongoni mwa sifa za wanawachuoni na wenye kutafuta elimu ya kisheria ni kuwa na subira na kuwapuuza wajinga na kuwa mpole na kusamehe ,si katika sifa za mwenye elimu kumjibu kila anayemsema au kuzungumza katika kila tukio kwa sababu hili huwenda likamletea madhara makubwa ya ambayo yatamfanya ajute majuto ambayo hatoyasahau katika maisha yake, mwenye kutafuta elimu ya kisheria anatakiwa ajipambe na tabia hii ya kuwapuuza wajinga au waovu na kama hajajipamba na tabia hii basi kuna faida gani ya kutafuta kwake elimu ?!.

قال تعالى :

Amesema Allah -aliyetukuka-:

     ﴿وَإِذَا خَاطَبَهُمُ 

ٱلْجَٰهِلُونَ قَالُواْ سَلَٰمًا﴾

Na wajinga wakisema nao (maneno mabaya) huwajibu : (maneno ya) Salama !

الفرقان 63

قال العلامة الشيخ صالح الفوزان -حفظه الله- :

Amesema mwanawachuoni mkubwa Swaleh Al-fauzan-Allah amuhifadhi-:

المراد بالجهل هنا :سوء الخلق لا الجهل الذي هو عدم العلم.

Makusudio ya ujinga hapa (ni) tabia mbaya si ujinga wa kutokuwa na elimu .

[شرح كتاب العبودية (١٩)

Funzo tunalopata hapa sisi wanafunzi wenye kusoma elimu ya dini inatakikana mtu kila anapozidi elimu na uchamungu wake uongezeke kwa sababu huyu Waki’i tunayemuelezea hapa alikuwa ni mwanawachuoni mkubwa kama alivyomuelezea imamu Ahmad-Allah amrahamu- pale aliposema :

ما رأيت أحدا أوعى للعلم ولا أحفظ من وكيع

“Sijapatapo kumuona yeyote mwenye kuikusanya zaidi elimu na wala mwenye kuhifadhi zaidi kuliko Waki’i ”

المصدر : سير أعلام النبلاء للذهبي.

Ufafanuzi wa maneno ya imamu Ahmad-Allah amrahamu- .

Hapa imam Ahmad-Allah amrahamu- ana msifu Waki’i kwa kule kuikusanya kwake elimu na tumeona namna elimu ilivyokuwa ikidhihiri athari yake katika matendo yake ,nasi tunamuomba Allah -aliyetukuka- aturuzuku elimu na tuifanyie kazi .
•┈┈┈┈••✦✿✦••┈┈┈┈•

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa : Mfungo pili 2 , 1445H =May 9, 2024M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
    •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *