Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net
قاعدة مهمة في معرفة البدع
KANUNI MUHIMU KATIKA KUIJUA BIDA’A
💎 قال العلامة ابن العثيمين رحمه الله:
Amesema Mwanachuoni
mkubwa ibn Uthaimin -Allah amrehemu-:
▪️الاستدلال بترك النبي صلى
الله عليه وسلم للشيء مع وجود سببه،
Kutumia dalili kwa kuacha kufanya kitu Mtume swala na salam za Allah ziwe juu yake pamoja na kuwepo sababu ya kufanya kitu hicho,
وأنه إذا ترك الشيء مع وجود سببه ؛ كان ذلك دليلا على عدم مشروعيته
na kwamba yeye (Mtume) atakapoacha kitu pamoja na kuwepo sababu ya kufanya kitu hicho hiyo inakuwa ni hoja ya kutokuwepo kitu hicho katika sheria /dini
وهذه قائدة مهمة : «كل شيء وجد سببه في عهد النبي صلى الله عليه وسلم ولم يشرع فيه النبي صلى الله عليه وسلم شيئا، فإحداث شيء له يعتبر بدعة»
na hii ni kanuni muhimu:
” Kila kitu ambacho ilipatikana sababu yake (ya kufanywa) katika zama za Mtume- swala na salam za Allah ziwe juu yake- na akawa hajaweka sheria yoyote ndani (ya kitu) hicho Mtume swala na salam za Allah ziwe juu yake- basi kumzushia chochote huyo (Mtume) kinazingatiwa ni bida’a .
وهذه قاعدة تنفعك ، ولها فروع كثيرة منها:
Na kanuni hii itakunufaisha na ina matawi mengi na miongoni mwayo ni:
🔺أن النبي صلى الله عليه وسلم كان إذا دخل بيته فأول ما يبدأ به السواك، فلو قال قائل إذا دخلنا المسجد هل تشرع البداءة بالسواك؛ لأن بيت الله
أعز من بیت الإنسان؟
(Mfano) : Kwamba Mtume- swala na salamu za Allah ziwe juu yake- alikuwa pindi anapoingia nyumbani kwake anaanza kupiga mswaki,
lau kama atasema msemaji : Pindi tunapoingia msikitini je ni sunnah kuanza kupiga mswaki ? ,kwa sababu nyumba ya Allah ni tukufu zaidi kuliko nyumba ya Mwanaadamu.
⏪ الجواب : لا يشرع للإنسان إذا دخل المسجد أن يتسوك. فاذا قال : أقيس ذلك على دخول البيت؟
Jawabu:
Si sunnah kwa mtu atakapoingia msikitini apige mswaki.
Na atakaposema:
nalinganisha huko (kuingia msikitini) na kuingia nyumbani.
قلنا: لا قياس في العبادات؛ والسبب مختلف: هذا دخول مسجد، وهذا دخول بيت؛
Tunasema: hakuna kulinganisha katika ibada, (ambazo) sababu ni tofauti:
hii ni kuingia msikitini na hii ni kuingia nyumbani
فلا قياس. ثم نقول: لو كان هذا مشروعا – أي التسوك عند دخول المسجد – لفعله النبي صلى الله عليه وسلم ؛ لأن السبب موجود.
Basi hakuna kulinganisha , kisha tunasema lau hili lingekua ni sunnah -yaani kupiga mswaki wakati wa kuingia msikitini-angelifanya Mtume swala na salam za Allah ziwe juu yake,kwa kuwa sababu ilikuwepo.
itaendelea inshaallah……
📚 شرح بلوغ المرام المجلد الثاني ص ١٦٥-١٦٦.
Maelezo ya mpitiaji:
Hii ni kanuni ya kujua jambo la uzushi katika dini :
Kila jambo ambalo sababu ya kufanywa ilikuwepo katika zama za Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie- na Mtume hakulifanya na wala hakuliamlisha lifanywe basi halifai kufanywa baada yake .
Mfano:
Mfano : Mtume- swala na salamu zimfikie- alifiwa na Mkewe bibi Hadijah ,na wanawe- Allah awaridhie- na haikopokewa kuwa aliwakusanya watu baada ya siku tatu au arobaini kwa ajili ya kusoma quran iwe ni dua kwa mkewe na wanaye ! na sababu ya kufanya ilikuwepo na kizuizi hakuna lakini hakufanya kwa hiyo kulifanya jambo hili ni uzushi katika dini.
Na mfano alioutoa shekhe -Allah amrahamu- wa kuwa ni suna mtu anapoingia nyumbani kwake anaanza kupiga mswaki lakini haikuthibiti kuwa ukiingia msikitini unaanza kupiga mswaki ama ukiwa unatawadha au unajiandaa na swala kupiga mswaki ni sunnah .
Imepitiwa na : Ismail Seiph Mbonde Asshafi’y
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Dhul-hijjah 26, 1442H ≈ August 5, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•