KANUNI MUHIMU KATIKA KUIJUA BIDAA
sehemu ya pili na ya mwisho:
Amesema mwanachuoni mkubwa ibn-Uthaimin
فحديث جابر رضي الله عنه يستدل به على هذه القاعدة العظيمة وهي:
Na hadithi ya Jaabir Allah amridhie hutolewa dalili juu ya kanuni hii tukufu :
” كل ما وجد سببه في عهد النبي صلى الله عليه وسلم ولم يفعله ففعله بدعة
“Kila kitu ambacho ilipatikana sababu ya kufanywa kwake katika zama za Mtume swala na salam za Allah ziwe juu yake na akawa hajakifanya basi kukifanya kitu hicho ni bidaa”
⚠️ هل يمكن أن نقول : وكذلك الاحتفال بمولد الرسول ؟
Je inawezekana tuseme:
Vilevile kusheherekea kuzaliwa kwa Mtume swala na salam za Allah ziwe juu yake ni ( bidaa?)
الجواب: نعم، نقول : إن الاحتفال بمولد الرسول صلى الله عليه وسلم بدعة بلا شك؛
Jawabu : Ndio, tunasema kwamba kusheherekea kuzaliwa kwa Mtume swala na salam za Allah ziwe juu yake ni bida’a (uzushi) bila shaka,
لأن سببه موجود في عهد النبي الله ولم يفعله،
kwa sababu sababu yake (ya kufanywa) ilikuwepo katika zama za Mtume swala na salam za Allah ziwe juu yake na hakufanya ,
ثم نقول : هل الرسول صلى الله عليه وسلم لا يعلم أنه سنة، أو يعلم أنه سنة ولم يبينه؟
Kisha tunasema: Je Mtume -swala na salamu za Allah ziwe juu yake- hajui kuwa ni sunnah au anajua kuwa ni sunnah na hakuibainisha?
وكلا الأمرين محال، محال أن يدخر الله تعالی علم هذا لمن يأتي بعد أربعمائة سنة ويحجبه عن رسول الله صلى الله عليه وسلم وخلفائه الراشدين،
Na yote mambo mawili ni muhali ni muhali Allah aiweke akiba elimu hii kwa yule aliyekuja baada ya miaka mia nne na aizuie (elimu) hiyo kwa Mtume swala na salam za Allah ziwe juu yake- na Makhalifa wake waongofu
ومن المحال أن يكون الرسول علمه ولم يبينه لأمته.
Na ni muhali awe Mtume swala na salam za Allah ziwe juu yake awe amefundishwa na asiubainishie ummah wake.
📚 شرح بلوغ المرام المجلد الثاني ص ١٦٥-١٦٦.
Maelezo ya mpitiaji tarjama:
Hadith ya Jabiri- Allah amridhie – ambayo sheikh anaikusudia ni hii tutakayoitaja hapa ,na kanuni hii aliitaja pindi alipokuwa akisherehesha hadithi hii :
عن جابرِ بنِ سَمُرَةَ قال : صلَّيتُ مع النَّبيِّ صلَّى اللَّهُ عليهِ وسلَّمَ غيرَ مرةٍ ولا مرتينِ العيدينِ بغيرِ أذانٍ ولا إقامةٍ
Kutoka kwa Jabir bin Samurah amesema:
Niliswali pamoja na Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie- zaidi ya mara moja na zaidi ya mara mbili (tuliswali) bila ya adhana wala iqamah .
أخرجه مسلم (٨٨٧)، وأبو داود (١١٤٨) واللفظ له، والترمذي (٥٣٢)، وأحمد (٢٠٨٤٧).
Kwa hiyo mwenye kuadhini au kukimu kabla ya swala ya eid atakuwa amefanya bida’a /uzushi, kwa sababu sababu ya kufanya hayo ilikuwepo na kulikuwa hakuna kizuizi kwa hiyo hii ni kanuni ya kujua bida’a /uzushi katika dini .
Sheikh -Allah amrahamu- ametoa mfano wa Maulidi yaani kuifanya siku au mwezi aliyozaliwa Mtume kuwa ni sikukuu ,jambo ambalo Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie- hakulifanya na wala Maswahaba na wala wanafunzi wa Maswahaba bali lilikuja kufanyika karne ya nne katika mwaka 363 baada ya hijra ,tena waliyoanzisha hii sikukuu ya Maulid ni Mashia ambao walikuwa na itikadi za kikafiri kabisa .
Imepitiwa na : Ismail Seiph Mbonde .
Imeandaliwa na: fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Muharram/Mfungo nne 6, 1443H ≈ August 14, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•