KANUNI NA MISINGI MUHIMU KATIKA KUISOMA SIRA YA MTUME -SWALA NA SALAMU ZA ALLAH ZIMFIKIE.

Makala namba (2)

للشيخ عبد الله بن صالح العبيد-حفظه الله-.

(Maneno ya) sheikh Abdullah bin Swaleh Al-ubaid -Allah amuhifadhi -.

مسائل مهمة في دراسة سيرة النبي -صلى الله عليه وسلم :

Masuala muhimu katika kusoma sira ya Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie – :

“ Hakika kanuni na msingi kwa wanachuoni wakubwa waliobobea na waliohifadhi katika maimamu wa wema waliopita katika kuyapokea yale yaliyonukuliwa kwa Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie -(sira) yamegawanyika sehemu kuu tatu :

Kigawanyo cha pili :

قسم اشتهر عند أهل العلم وضمن في بعض المسانيد وبعض السنن كالسنن الأربعة وكذلك المسانيد كمسند الإمام أحمد ومسند الدارمي وأشباه ذلك من المسانيد.

Ni kigawanyo ambacho kimekuwa mashuhuri kwa wanavyuoni na (matukio hayo ya sira) yakawekwa katika baadhi ya (vitabu vya hadithi) vya masaaniid na baadhi ya sunan kama vile sunani nne na masaaniid kama vile musnad imam Ahmad na musnad Addaarimiy

ومن هذا القسم الثاني : هذا الذي اشتهر عند أهل العلم وإن لم يكن فيه أعلى درجات الصحة

Na katika kigawanyo hichi (cha pili pia) : Ni haya (matukio) yaliyokuwa mashuhuri kwa wanawavyuoni na hata kama hayana daraja la juu zaidi la usahihi

إلا أنه أخذ مأخذ القبول : سيرة ابن إسحاق التي هذبها ابن هشام زاد فيها أشياء من غير قليل وحذف منها أشياء قليلة كبعض الأشعار يقطع بأنها منحولة مثلا برأي ابن هشام.

Isipokuwa yamepewa nafasi ya kukubaliwa (mfano yale yaliyomo katika ) : Sira ya ibn Is-haq ambayo aliipembua ibn Hisham aliongeza vitu ambavyo si vichache na akaondosha vitu vichache kama vile baadhi ya mashairi yaliyonasibishwa kwa watu wasiokuwa wenyewe kwa rai ya ibn Hisham.

Maelezo ya mfasiri :

Kisha sheikh alieleza kuwa kigawanyo hichi cha pili na yeye alikitilia nguvu yaani hichi kigawanyo ambacho hakina daraja la juu zaidi la usahihi lakini ni mashuhuri na kimekubaliwa kwa maimamu wakubwa waliohifadhi riwaya na kwa ajili hii utaona vitabu vya sira ambavyo vimekuwa mashuhuri baina yao Kama vile cha : Azzuhriy na Musa bin ‘Uqubah, na ibn Is-haqah, na ibn Hisham na mfano wa vitabu hivyo. Wote hao wamekipokea kigawanyo hichi kwa kukikubali (walikuwa) wakikisoma na wakikieneza na utavikuta vitabu vyao vimeenea katika miji mbalimbali ya kiislamu na maana ya kukubalika kwa aina ya matukio haya mashuhuri ya sira ambayo yamepokewa kwa riwaya ni kwa sababu wao wameyapokea kwa kusimuliana (isnad) kizazi baada ya kizazi na huu umashuhuri kwao unachukua nafasi ya kukubalika.

Ama yule atakayetaka kukikosoa kigawanyo hichi mashuhuri ambacho wamekipokea hao wanachuoni wakubwa kwa kukikubali kufanya hivi ni kinyume na njia ya wanachuoni hao na mwenye kufanya hivyo hatoweza kuyanasibisha maneno yake kwa yeyote katika wanachuoni hao kama vile imamu Ahmad, Al-bukhariy, Ashaafiy, Malik, Abuu Hanifah, Annawawiy, Al-auza’iy, Abuu Hatim na wengineo wasiokuwa hawa, na hivi vitabu vimeandikwa zama zao na wakaweka sehemu kubwa ya aina za riwaya hizi mashuhuri ambazo hazina daraja la juu zaidi la usahihi kwa hivyo kuzikataa riwaya hizi si sawa.

Na mfano wa matukio haya mashuhuri ambayo yamepokelewa kwa kukubaliwa na maimamu wa wema waliopita ni tukio la bibi Khadijah -Allah amridhie – kuolewa akiwa na miaka arobaini.

Kwa hiyo katika sira wanachuoni hawakuweka sharti la usahihi wa riwaya bali hutosheka na umashuhuri wa riwaya ila katika yale yanayohusiana na masuala ya itikadi au kuthibitisha hukumu ya kisheria muda huo kutawajibika kuzipembua riwaya kama alivyosema imam Ahmad-Allah amrahamu -:

” إذَا جَاءَ الْحَلَالُ وَالْحَرَامُ شَدَّدْنَا فِي الْأَسَانِيدِ ; وَإِذَا جَاءَ التَّرْغِيبُ وَالتَّرْهِيبُ تَسَاهَلْنَا فِي الْأَسَانِيدِ“

Inaendelea Allah akitaka

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo tatu 10, 1443H ≈ Jul 9, 2022M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
    •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *