KANUNI ZA SHAKA KATIKA SWALA (2).

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net

🔺 قواعد الشك في الصلاة.

KANUNI ZA SHAKA KATIKA SWALA

sehemu ya pili (2)

◾️ قال العلامة ابن عثيمين رحمه الله:

Amesema mwanachuoni mkubwa ibn Uthaimin -Allah amrehemu-:

⏪ القاعدة الثانية: إذا كان الشَّكُّ وهو، أي: طرأ على الذِّهن ولم يستقر،

Kanuni ya pili:

Itakapokua shaka imejitokeza katika akili na haijatulizana,

كما يوجد هذا في الموسوسين، فلا عِبْرَة به أيضاً، فلا يلتفت إليه، والإِنسان لو طاوع التوهم لتعب تعباً عظيماً.

kama linavyopatikana hili kwa wale wenye (maradhi ya) wasiwasi,basi (shaka hii) haizingatiwi vilevile, (yaani) asiigeukie (asiizingatie), na mwanadamu lau kama angezitii fikra /mawazo (basi) angepata tabu sana.

⏪ القاعدة الثالثة: إذا كَثُرت الشُّكوك مع الإِنسان حتى صار لا يفعل فِعْلاً إلا شَكَّ فيه،

Kanuni ya tatu:

Pindi shaka zitakapokithiri kwa mtu mpaka akawa hafanyi kitendo chochote isipokua huwa na shaka ndani yake,

إنْ توضأ شَكَّ، وإنْ صَلَّى شَكَّ، وإن صام شَكَّ، فهذا أيضاً لا عِبْرَة به؛

ikiwa atatawadha anakua na shaka, ikiwa ataswali anakua na shaka,ikiwa atafunga anakua na shaka ,basi (shaka) hizi vilevile hazizingatiwi,

لأن هذا مرض وعِلَّة، والكلام مع الإِنسان الصَّحيح السَّليم مِن المرض، والإِنسان الشكّاك هذا يعتبر ذهنه غير مستقر فلا عِبْرَة به.
Kwa sababu huu ni ugonjwa na kasoro, (ama hapa) maneno (yanamhusu) mtu aliye mzima wa afya, ambaye amesalimika na maradhi.

(Ama) mtu ambaye ana shaka nyingi huyu anazingatiwa akili yake haijatulizana na haizingatiwi shaka kwake.

📚 [ الشرح الممتع 2/308 ].

Maelezo ya mpitiaji:

Hii ndiyo hukumu ya shaka katika swala ikiwa mtu ametokewa na shaka kama alivyoeleza sheikh -Allah amrahamu ,

ama katika madhehebu (ya kishafii) , shaka ndani ya swala ni kama yakini, maana yake ni hii:

Mfano ulikuwa ukiswali swala ya adhuhr kisha ukawa na shaka je hii ni rakaa ya kwanza au ya pili ?

Jawabu: Hii ni rakaa ya kwanza hata kama baadae dhana yako yenye nguvu ikikuambia kuwa hii ni rakaa ya pili ,kwa maana ukiwa na shaka ya nguzo katika swala basi hukumu yake hiyo nguzo haujaifanya na kama ni rakaa utajengea uchache kama una shaka je hii ni rakaa ya tatu au ya nne hiyo itakuwa ni ya tatu .

Kwa maana hatutumii kanuni ya kuchukua dhana yenye nguvu inayosema:

الْمَظِنَّةُ لَهَا حُكْمُ الْمَئِنَّةِ

“Dhana ina hukumu ya yaqini” .

Kanuni hii haitumiki katika swala katika madhehebu (ya kishafii).

Hukumu ya mtu mwenye maradhi ya wasiwasi/ shaka nyingi:

kanuni inasema:

الشّكُّ لا يُعْتَبَرُ مِنْ كَثِيْرِ الشُّكُوْكِ

” Shaka haizingatiwi kwa mwenye shaka nyingi “

Mtu ambaye kila anachofanya huwa na shaka kwa maana mwenye wasi wasi uliomzidi akawa kila anacho kifanya huwa na shaka mtu huyu shaka yake hatoizingatia

Mfano akawa kila anapotawaza au anaposwali anajiwa na shaka na pia katika ibada nyingine :

Mfano akawa ana swali ikamjia shaka jee hii ni rakaa ya tatu au ya nne ?

Jawabu: Hii ni ya nne ,kwa sababu yeye ni mgonjwa.

Mfano akawa anatawadha na alipoosha miguu ikamjia shaka : Je nimepaka kichwa ?

Jawabu: Umepaka kichwa ,kwa sababu huyu ni mgonjwa wa wasiwasi .

Na pia katika ibada nyinginezo msingi ni huu huu yaani kwa mwenye maradhi ya wasiwasi na wingi wa shaka .

Mpitiaji: Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Swafar/Mfungo tano 23, 1443H ≈ September 30, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *