KATIKA ADA ZILIZOKUWEPO TOKEA KALE NI KUWANENEPESHA MABINTI WANAOANDALIWA KWA AJILI YA KUOLEWA

عن عائشة رضي الله عنها قالت :

Kutoka kwa ‘Aisha -Allah amridhie- amesema-:

(أَرَادَتْ أُمِّي أَنْ تُسَمِّنَنِي لِدُخُولِي عَلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ

Mama yangu alitaka kuninenepesha kwa ajili ya kuingia kwa Mtume wa Allah – swala na salamu ziwe juu yake – (baada ya kunioa)

فَلَمْ أَقْبَلْ عَلَيْهَا بِشَيْءٍ مِمَّا تُرِيدُ حَتَّى أَطْعَمَتْنِي الْقِثَّاءَ بِالرُّطَبِ فَسَمِنْتُ عَلَيْهِ كَأَحْسَنِ السَّمْنِ) .

basi sikumkubali (mama yangu kwa) kutumia chochote (alichotaka katika dawa) mpaka akanilisha matango kwa kuchanganya na tende mbivu basi nikanenepa kwa sababu ya (vyakula) hivyo unene mzuri “

رواه أبو داود (٣٩٠٣)

Maelezo ya mtarjumu:

Kawaida ya kuwanenepesha wana wali yaani wanawake wanaojiandaa kuolewa baada ya kuposwa ,kawaida hii ilikuwepo tokea kale kama anavyoelezea mama yetu Aisha -Allah amridhie- kuwa mama yake alikuwa akimuandaa kwa ajili ya kuolewa na mtume kwa kumnenepesha na alitaka kumlisha madawa mbalimbali ili awe mnene lakini mama Aisha -Allah amridhie- alikuwa akijisikia unyonge kwa maana alikuwa hapendi kutumia hizo dawa mpaka pale mama yake alipomtengenezea matango yaliyochanganywa na tende mbivu ikiwa ndiyo sababu ya kunenepa vizuri.

Na wanachuoni wa tiba wanasema kuwa :

Katika tende mbivu kuna (asili ya) joto , na katika tango kuna (asili) ya baridi kwa hiyo vikichanganywa viwili hivi hupatikana chakula cha hali ya kati na kati .
Kwa hiyo katika faida za kula vyakula vya mchanganyiko huu vina saidia kuweka hali sawa na kunenepesha mwili.

Angalia :تحفة الأحوذي

Tanbih:

Matango yanayokusudiwa hapa ni yale yenye mistari mistari iliyochimba na wala si haya matango ya kawaida ,matango haya ni yale yanayoitwa kwa kiarabu (الْقثّاء) na wala si (الخيار)

Mfasiri : Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo saba 16, 1443H ≈ November 21, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *