Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net
KATIKA SABABU ZA KUPATA UTULIVU NA RAHA KATIKA MAISHA !
↩ الزوجة_الصالحة.
Mke mwema
🎙قال الشيخ عبدالرزاق_البدر -حفظه الله
Amesema sheikh Abdul-Rrazzaq Al-Badr-Allah amuhifadhi-:
ومن أسباب السعادة:
الزوجة الصالحة في بيت الانسان، إذا أكرم الله تعالى الانسان في بيته بزوجة صالحة: هذا من أسباب السعادة.
Na miongoni mwa sababu za utulivu/raha :
Ni mke mwema katika nyumba ya mwanadamu ,pindi -Allah aliyetukuka- atapomkirimu mwanadamu katika nyumba yake mke mwema (basi) hii ni katika sababu za utulivu.
📍ومن أسباب الشقاء :
أن يُبتلى الانسان في بيته بزوجة ليست صالحة، هذا من أسباب الشقاء.
Na katika sababu za tabu/shida:
Ni mwanadamu kupewa mtihani nyumbani kwake kwa wa mwanamke asiyekuwa mwema ,hii ni katika sababu za tabu.
⚪ لأن بيت الانسان سكنه وموضع راحته، وطمأنينته، وسكون نفسه بعد معاناة العمل والاحتكاك بالناس والقيام بما يقوم به الانسان من صناعة، أو نحو ذلك،
Kwa sababu nyumba ya mwanadamu ni makazi yake, na ni sehemu yake ya kupumzika ,na ni utulivu wake ,na ni (sehemu) ya kutulizana nafsi yake baada ya kuhangaika na kazi na kuchanganyika na watu , na (baada) ya kuyafanya yale anayoyafanya mwanadamu kama vile (shughuli za) ufundi au mfano wa hizo ,
فإذا رجع إلى البيت احتاج إلى السكن، فإذا كان في البيت امرأة صالحة تقيّة تخاف الله -جل وعلا- وتتقي الله في زوجها: كان هذا من أسباب سعادته وقرة عينه.
basi pindi ataporudi nyumbani huitajia utulivu,basi kukiwa katika nyumba kuna mwanamke mwema mcha Mungu mwenye kumuogopa Allah- aliyeshinda na kutukuka-na (akawa) anamcha Allah kwa upande wa mumewe ,linakuwa hili ni katika sababu za furaha yake na kiburudisho cha macho yake .
📚 شرح رسالة ابن القيم إلى أحد اخوانه (-٢-).
Maelezo ya mfasiri:
Amesema kweli sheikh -Allah amuhifadhi- bila shaka mwenye kupata mke mwema amepata utulivu na raha katika maisha yake , kama alivyosema Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie-:
الدُّنْيَا مَتَاعٌ ، وَخَيرُ مَتَاعِهَا المَرْأَةُ الصَّالِحَةُ
” Dunia ni starehe fupi yenye kuondoka na bora ya starehe zake ni mke mwema “
رواه مسلم
Na vilevile katika hadithi nyingine pale Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie- aliposema kuwa mambo manne ni katika raha ya dunia la kwanza kulitaja ni :
” المرأةُ الصالحة…”
” Mke mwema…”
na vilevile akataja mambo manne ni katika tabu na shida za dunia na la kwanza kulitaja ni:
” المرأة السوء…”
” Mke muovu …”
Kwa hiyo mke mwema ndiyo msingi wa raha na utulivu wa mwanamume katika maisha yake , lakini ili upate mke mwema wewe mwenyewe kwanza uwe mwema ama ukiwa muovu bila shaka hata ukimpata hamtodumu.
Mfasiri: Ismail Seiph Mbonde
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Dhul-hijjah 24, 1442H ≈ August 3, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•
Mashaallah!