Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net
KAULI ZA WANACHUONI KUHUSU USALAFI /NJIA YA WEMA WALIOPITA .
قال الشيخ مُقبل بن هادي الوادعيّ، رَحِمَهُ اللهُ تَعَالَى:
Amesema sheikh Muqbil bin Haad Al-waadi’iy -Allah amrahamu:
“فإذا أحببنا أننا نقول :
سلفيون ،
Basi kama sisi tunapenda kusema:
Sisi ni wenye kujinasibisha na wema waliopita,
لا بدّ أنْ ندرس سيرة السَّلف،
وأن نقتدي بسلفنا،
Hatuna budi kuisoma mienendo ya wema walio pita,
Na tuwafuate wema wetu walio pita,
لسنا نكتفي بادّعاء السَّلفيّة؛
وبالدِّعاء السنيةوالسلفية “
tusitosheke na kudai usalafi;
na kudai usuni na usalafi.
📚 إجابة السّائل على أهمّ المسائل (ص: ٣٧٤)
[ Ijaabatu ssaail ‘alaa ahammi l-masaail, ukurasa (374) ]
Maelezo ya mwandishi: 🎤
Usalafi /kuwafuata wema waliopita si kujinasibisha tu, bali ni matendo, unaweza ukajinasibisha, lakini ukawa haumo bali yakawa ni madai tuu, mazingatio ni kufuata kwa vitendo sio kujiita tu!, nasaha hizi za sheikh Muqbilu- Allah amrahamu- zinafanana na nasaha za wengine katika wanachuoni kama vile mwanachuoni mkubwa wa fiqih ibn Uthaimin-Allah amrahamu- : pale aliposema
ويلزم من كوننا نحث الطلبة على منهج السلف، يلزم من ذلك تحريضهم على معرفة منهج السلف،
Inalazimika kuwahimiza kwetu wanafunzi juu ya (kufuata) njia ya (wema) waliopita, na inalazimika kutokana na hilo kuwahimiza juu ya kuijua njia ya wema waliopita,
فنطالع الكتب المؤلفة في ذلك، كـ (سير أعلام النبلاء)، وغيرها حتى نعرف طريقهم، ونسلك هذا المنهج القويم.
(tuwaambie) basi tusome vitabu vilivyotungwa katika hilo kama vile (siyaru ‘alaami nnubalaa) ,na vinginevyo ili tujue njia yao na tupite njia hii iliyonyooka .
انظر : شرح حلية طالب العلم .
Na vilevile sheikh Fauzan-Allah amuhifadhi- katika muhadhara wake maarufu -Njia ya wema waliopita na hitajio la uma la njia hiyo – ,miongoni mwa yale aliyoyazungumza baada ya kuhimiza kuifahamu njia ya wema waliopita kwa kuisoma kisha akasema :
وأما مجرّد الانتساب إلى السلف والسلفية من غير معرفة بها وبمنهجها فهذا لا يجدي شيئا ؛ بل قد يضر، لا بد من معرفة منهج السلف الصالح .
Ama kujinasibisha tu kwa (wema) waliopita ,na (kujinasibisha) na usalafi bila ya kuujua na (kuijua) njia yake basi hili halinufaishi chochote ,bali huwenda likadhuru, hakuna budi kuijua njia ya wema waliopita .
══════ ❍ ✿ ❍ ══════
Ufafanuzi wa mwandishi:
Bila shaka madhara ya kutoifahamu vilivyo njia hii ya wema waliopita ni makubwa mno huwenda kuna baadhi ya waislamu wakaichukia njia hii kwa sababu ya baadhi ya matendo ya wajinga wanaojinasibisha na njia hii bila ya elimu ! .
Wengine wanadhani kuwa usalafi umejengeka kwa kukosoa tu yaani kuradi bila ya kuangalia maslahi katika hilo ! , wengine wanadhani kuwa usalafi umefungwa na mtu fulani au sehemu fulani ukiafikiana nao katika kila jambo basi wewe umo katika mstari na kama ukitofautiana nao basi wewe umetoka hata kama ni jambo ambalo halimtoi mtu katika sunnah !.
makosa haya na mengine hayatoondoka bila ya kusoma kwa wajuzi na kuwasikiliza wanachuoni waliobobea katika elimu na walioishi katika njia hii, wale wa kale na wanachuoni wetu wa zama hizi kama vile : Sheikh ibn Baaz ,sheikh Al-albaniy,sheikh ibn Uthaimin- Allah awarahamu – na wengineo wengi waliokufa -Allah awarahamu- na waliokuwa hai -Allah awahifadhi-.
Usalafi/ njia ya wema waliopita ni ule uislamu aliokuja nao Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie- njia hii inawalingania waislamu wawe wamoja maadamu ni muislamu aliyeshikamana na qurani na sunnah na ameshikamana na njia ya Maswahaba basi huyo tunampenda mia kwa mia na ni ndugu yetu popote alipo tumjue au tusimjue .
Na waislamu wengine ambao hawapo katika njia hii tunawapenda kwa kadri ya imani zao na tunawachukia kwa bida’a zao pamoja na kuwaonea huruma kwa upotevu waliokuwa nao na kuwalingania katika haki kwa njia mzuri .
Mwandishi: Ismail Seiph Mbonde Assha’afiy
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Muharram/Mfungo nne 4, 1442H ≈ August 12, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•