KISA CHENYE MAZINGATIO CHA KIJANA MWENYE KUMUOGOPA ALLAH!

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net

KISA CHENYE MAZINGATIO CHA KIJANA MWENYE KUMUOGOPA ALLAH!

عن سفيان -رحمه الله – قال :

Kutoka kwa Sufiani -Allah amrahamu – amesema :

بلغنا أن أم الربيع كانت تنادي

  • فتقول : يابني، يا ربيع، ألا تنام !

Imetufikia (habari) kuwa mama Arrabi’i alikuwa akinadi akisema :Ewe mwanangu mpenzi, ewe Arrabi’i hivi haulali ?

  • فيقول : ياأماه من جن عليه الليل وهو يخاف البيات حق له أن لاينام .

Basi (yule mtoto) husema :

Ewe mama yangu ,yule aliyefikiwa na giza la usiku na hali ana hofu na umauti ni haki kwake asilale .

قال : فلما بلغ ورأت ما يلقى من البكاء والسهر نادته
فقالت :

(Sufian) alisema : Basi pindi alipozidisha (kukesha) na (mama) akaona ile (tabu) inayompata (mwanaye) katika kulia na kukesha ,basi (mama) akasema :

يا بني لعلك قتلت قتيلاً ؟!

  • فقال : نعم يا والدة ، قتلت قتيلاً !!

Ewe mwanangu mpenzi huwenda (ukawa) umemua uliyemua ?!

Basi (Arrabi’i) akasema : Ndiyo ewe mama ,nimemua yule niliyemua !!

فقالت : ومن هذا القتيل يا بني نتحمل على أهله فيعفوك

Basi (mama yake) akasema : Ni nani huyu uliyemuua ewe mwanangu mpenzi (ili) tujikalifishe (tukazungumze na) jamaa zake wapate kukusamehe.

والله لو علموا ما تلقى من البكاء والسهر لقد رحموك .

Na namuapia Allah lau wangejua yale (mashaka) unayoyapata katika kulia na kukesha bila shaka wangekuonea huruma.

  • فيقول : ياوالدتي هي نفسي
    قتلتها بالمعاصي !

Basi (Arrabi’i) husema : Ewe mama yangu hiyo ni nafsi yangu nimeiua kwa maasi!

صفة الصفوة(1/313)

Maelezo ya mfasiri :

Huyu ndiye Arrabi’i bin Khuthaim – Allah amrahamu – ambaye alikuwa ni katika taabi’in kwa maana alikuwa ni katika wale waliowadiriki na kuwawahi Maswahaba na akajifunza kwao na huyu alikuwa ni mtu wa karibu zaidi wa ibn Masud -Allah amridhie – ,huyu Arrabi’i bin Khuthaim alikuwa ni katika watu wenye kupigiwa mfano katika ucha Mungu na katika ibada zake alizokuwa akishikamana nazo ni kisimamo cha usiku na bila Shaka kusimama usiku ni katika sifa za wacha Mungu kama alivyoeleza Allah katika suratul -Adh-dhaariyat pindi alipotaja miongoni mwa sifa za wacha Mungu :

كَانُواْ قَلِيلًا مِّنَ ٱلَّيْلِ مَا يَهْجَعُونَ {١٧}

Walikuwa wakilala kidogo tu usiku.

وَبِٱلْأَسْحَارِ هُمْ يَسْتَغْفِرُونَ {١٨}

Na wakiomba msamaha nyakati za kabla ya alfajiri.

Suratu Ad-dhaariyat : 17-18.

Na kisimamo cha usiku kinafaida nyingi kama alivyosema Mtume -swala na salamu zimfikie- :

عليكُم بقيامِ اللَّيلِ ، فإنَّهُ دَأْبُ الصَّالِحينَ قبلَكُم ،

Jilazimisheni na kisimamo cha usiku, hakika hicho (kisimamo) ni kawaida ya watu wema waliopita kabla yenu,

و قُربةٌ إلى اللهِ تعالى ومَنهاةٌ عن الإثمِ و تَكفيرٌ للسِّيِّئاتِ ، ومَطردةٌ للدَّاءِ عن الجسَدِ

na ni ibada inayomkurubisha (mja) kwa Allah – aliyetukuka-, na ni chenye kuzuia madhambi, na ni chenye kufuta makosa ,na ni chenye kuondoa maradhi katika mwili.

صحيح الجامع

Hizi ni miongoni mwa faida za kisimamo cha usiku.

Pia tunajifundisha kuwa muumini anatakiwa amuabudu Allah kwa kuogopa na kutaraji ,kama tunavyoona kwa mwema huyu pamoja na ucha Mungu aliokuwa nao na kutaraji kuwa Allah atamuingiza peponi lakini anaiona nafsi yake kuwa ni yenye makosa na madhambi! na hii ndiyo kawaida ya watu wema siku zote huzituhumu nafsi zao kuwa ni zenye mapungufu!.

Pia katika kisa hiki kuna mazingatio makubwa kwa vijana, na mahimizo ya kumcha Allah katika ujana wao na wala wasihadaike na dunia na ujana wao.

Mwisho nawausia ndugu zangu waislamu tutenge muda haswa kabla kidogo ya al-fajir kwa ibada mbalimbali na haswa kumtaka Allah msamaha kwa madhambi tuliyoyafanya, na jitahidi muda huu wa kabla ya kuingia al-fajiri kwa dakika chache uwe unamuomba Allah msamaha usijishughulishe na ibada nyingine muda huu, na kufanya hivyo ni bora zaidi kwako.

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo pili 5, 1443H ≈ Jun 5, 2022M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *