KISA KIZURI KATIKA KUELEZEA USAFI WA MOYO.

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net

قِصَّةٌ رَائِعَةٌ فِي صفاءالقلب

Kisa kizuri katika (kuelezea) usafi wa moyo.

” كان طلحة بن عبدالرحمن بن عوف أجود قريش في زمانه
فقالت له امرأته يوما :

Alikuwa Twalha bin Abdul-Rrahman bin ‘Auf ni Mkuraishi mkarimu zaidi katika zama zake ,basi siku moja mkewe alimwambia (hivi):

ما رأيت قوما أشدّ لؤْما منْ إخوانك .
قال : ولم ذلك ؟

Sijapatapo kuona watu wenye lawama zaidi kuliko ndugu zako .

(Twalha ) akamuuliza: Kwa sababu gani (unazungumza) hayo ?

قالت : أراهمْ إذا اغتنيت لزِمُوك ، وإِذا افتقرت تركوك !

(mke) akasema: Nawaona pindi unapokuwa unauwezo wanashikamana na wewe ,na pindi unapokuwa fakiri wanakuacha !

فقال لها : هذا والله من كرمِ أخلا‌قِهم ! يأتوننا في حال قُدرتنا على إكرامهم..

basi (Twalha) akamwambia: Hili (wanalolifanya) naapa kwa Allah ni katika uzuri wa tabia zao !wanatujia katika hali (ambayo) tunauwezo wa kuwakirimu ..

ويتركوننا في حال عجزنا عن القيام بِحقهم ” .

na wanatuacha katika hali tunayoshindwa kusimamia haki zao (kama kuwakirimu ,n.k)”.

علّق على هذه القِصة الإ‌مام الماوردي الشافعي فقال :

Imamu Al-mawardiy Asshafiy alikiwekea maelezo mafupi kisa hiki akasema:

” انظر كيف تأوّل بكرمه هذا التأويل حتى جعل قبيح فِعلهم حسنا ، وظاهر غدرِهم وفاء .

(Hebu) tezama vipi ametafsiri (vitendo vyao) tafsiri hii kwa ukarimu (alionao) mpaka akajalia vitendo vyao vibaya kuwa ni vizuri , na (akajaalia) udhahiri wa hiyana yao kuwa ni utekelezaji

وهذا والله يدل على أنّ سلا‌مة الصدر راحة في الدنيا وغنيمة في الآ‌خرة وهي من أسباب دخول الجنة

na (tendo) hili naapa kwa Allah linajulisha kuwa kusalimika kwa moyo ni (sababu ya) raha duniani na ni ngawira (huko) akhera ,na (tendo) hilo ni katika sababu za kuingia peponi .

Amesema Allah aliyetukuka

( وَنَزَعْنَا مَا فِي صُدُورِهِم مِّنْ غِلٍّ إِخْوَانًا عَلَىٰ سُرُرٍ مُّتَقَابِلِينَ ) “.

{Na tutaondoa chuki iliyokuwa vifuani mwao, na (watakuwa) ndugu (wenye kupendana) (waliokaa) juu ya viti vya kifalme ,wameelekeana (wanazungumza kwa furaha kubwa).

سورة الحجر ٤٧

[أدب الدنيا والدين ( ص ١٨٠ ).

🌸🌸

Maelezo ya mtarjumu:

Maana ya hiyo aya ni kuwa watu kabla ya kuingia peponi watasafishwa hawatokuwa na chuki ,mifundo ,na bughudha baina yao bali watakuwa ni ndugu na wataishi kwa raha na furaha, na usafi wa moyo na kusalimika na maradhi yake ni katika sababu za kuingia peponi, na miongoni mwa maradhi ya moyo ni: Husuda,chuki,mifundo,kuwadhania watu dhana mbaya bila ya sababu .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Swafar/Mfungo tano 7 ,1443H ≈ September 14, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *