KIUNGO CHA KUTILIWA UMUHIMU ZAIDI KATIKA MWILI!

◾️ قال العلامة العثيمين رحمه الله:

Amesema mwanachuoni mkubwa ibn Uthaimin- Allah amrahamu-:

أهم شيء هو حضور القلب ، إذ إن عمل الجوارح سهل على كل أحد، حتى المنافق يمكن أن يعمل عمل الجوارح،

Kitu muhimu zaidi ni kuhudhuria moyo, kwa sababu matendo ya viungo ni mepesi kwa kila mtu hata mnafiqi anaweza kutenda matendo ya viungo,

لكن الشأن كل الشأن هو في عمل القلب ، وحضوره ، وصحته، وسلامته،

Lakini mambo yote (yapo) katika matendo ya moyo , na kuhudhuria (kwake) na uzima wake na usalama wake,

ولهذا يجب علينا أن نعتني بقلوبنا: بأعمالها، وإراداتها، واعتقادها.

Na kwa ajili hii inawajibika juu yetu tutilie umuhimu nyoyo zetu , matendo yake ,na matashi yake, na itikadi yake.

📚 [التعليق على صحيح مسلم (٥٠٩/٤)

Maelezo ya mfasiri :

Moyo unapotengemaa basi viungo vyote hutengemaa kama alivyosema Mtume-swala na salamu za Allah zimfikie-:

ألا وإنَّ في الجَسَدِ مُضْغَةً، إذا صَلَحَتْ، صَلَحَ الجَسَدُ كُلُّهُ،

Sikilizeni, na bila shaka katika mwili kuna kipande cha nyama, pindi kitakapotengemaa hutengemaa mwili wote,

وإذا فَسَدَتْ، فَسَدَ الجَسَدُ كُلُّهُ، ألا وهي القَلْبُ.

Na kitakapoharibika hutaharibika mwili wote, sikilizeni na hicho (kipande) ni moyo .

متفق عليه.

Yale yaliyopo katika nyoyo ndiyo kipambanuzi baina ya muislamu wa kweli yaani muumini na baina ya mnafiqi ambaye hudhihirisha uislamu na kuficha ukafiri .

Na siku ya kiama yatadhihirishwa yote yaliyopo katika nyoyo na kuwekwa wazi kama alivyosema Allah -aliyetukuka- :

{ يَوْمَ تُبْلَى ٱلسَّرَآئِرُ }

Na siku zitakapotahiniwa siri (zikadhihirishwa ).

سورة الطالق ٩

Kwa hiyo tunatakiwa tuzichunge nyoyo zetu tufanye matendo kwa ajili ya Allah, na tuzitakase nyoyo zetu na maradhi yaliyojificha kama vile :Unafiqi, husuda,chuki,mafundo n.k ,na nyoyo zetu ziwe salama kwa waislamu wenzetu.

Napia tutilie umuhimu matendo ya nyoyo kama vile kutegemea ,kuogopa,kujikinga, na pia tuyaangalie yale matashi ya nyoyo zetu na nia zake,yote haya tuyafanye kwa ajili ya Allah, na kabla ya yote haya itikadi zetu ziwe sahihi.

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo tano 4, 1443H ≈ Aug 31, 2022M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *