Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiya.net
KUFA NA TAUHIDI NI SABABU YA KUPEWA TAUFIQ YA KUJIBU MASWALI YA KABURINI.
قال الله عزوجل :
Amesema Allah- aliyeshinda na kutukuka:
يُثَبِّتُ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا بِالْقَوْلِ الثَّابِتِ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَفِي الْآخِرَةِ
{{Allah huwathibitisha wale walioamini kwa kauli thabiti, katika maisha ya dunia na katika akhera }}.
سورة إبراهيم ٢٧
🍃والقَولُ الثَّابتُ هُو كلمةُ التَّوحيد
الّتي ثبتَت فِي قَلب المُؤمِن بِالحجَة والبرهَان
Na kauli thabiti /imara ni tamko la tauhid /kupwekesha ,(tamko) ambalo limethibiti katika moyo wa muumini kwa hoja na hoja ya yaqini .
🍃 وتّثبِيت المُؤمِنين بهَا فِي الدّنيَا ، أنَّهم يَتمسكُون بِها ولو نَالهم فِي سَبيلها مَا نالهُم من الأذى والتعْذيب
🍃 وتثْبيتُهم بهَا فِي الآخرةِ توفيقهم لِلجواب عِند سُؤال المَلَكَينِ .
Na kuwathibitisha (waumini) na tamko hilo katika dunia ni kuwa (waumini) watashikamana na (tamko) hilo na hata kama watapatwa katika njia ya (kushikamana na) hilo yale yatakayowapata katika maudhi na kuadhibiwa .
Na kuthibitishwa na (tamko) hilo akhera ni kupewa taufiq ya kujibu pindi watakapoulizwa (maswali ) na Malaika wawili.
📚 العلامة الفوزان حفظه الله /شَرح العَقِيده الوَاسِطيَّة : (١٨٢)
Maelezo ya mfasiri :
Hiyo ndiyo maana ya aya hii, Allah huwathibitisha waumini katika maisha ya dunia akawakinga na maradhi ya utata na matamanio machafu kwa sababu ya tauhidi yao waliyokuwa nayo na wakathibiti juu ya imani pamoja na mitihani watakayoipata,na pia huwathibitisha akhera yaani kaburini wakawa na uwezo wa kujibu maswali watapoulizwa na Malaika, kwa maana makusudio ya akhera katika aya hii ni kaburini na hiyo ndiyo kauli ya wanachuoni wengi zaidi wa tafsiri .
Muandaaji: fawaidusalafiya.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiya.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Shawwal 24, 1442H ≈ Jun 4, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•