KUINGIZA FURAHA KATIKA MOYO WA MUISLAMU.

قيل للتابعي الجليل محمد بن المنكدر رحمه الله :

Aliaulizwa tabi’y mtukufu Muhammad bin Al-Munkadir -Allah amrehemu -:

أيُّ الدنيا أعجب إليك ؟

قال : إدخال السرور على المؤمن

Dunia ipi inapendeza zaidi kwako?

Akajibu : Kuingiza furaha kwa muumini

قضاء الحوائج لابن أبي الدنيا ٣٣

Maelezo ya mfasiri :

Huyu ni mmoja katika mataabi’in yaani ni katika wale waliowawahi Maswahaba na wakajifunza kutoka Kwao , na hapa aliulizwa kuwa ni jambo gani linalomvutia na kupendeza zaidi kwake duniani ?

akasema kuwa :Ni kumfanyia muislamu jambo ambalo litamfanya awe na furaha kwa maana ni kuingiza furaha katika moyo wa muumini.

Na bila shaka kuna maneno yamekuja kutoka kwa Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie -katika hadithi ndefu kidogo ambayo baadhi ya wanachuoni wamehukumu kuwa ni hadithi nzuri :

” …وأَحَبُّ الأعمالِ إلى اللهِ عزَّ وجلَّ سرورٌ تُدخِلُه على مسلمٍ..“

Na matendo yanayopendeza zaidi kwa Allah -aliyeshinda na kutukuka – ni furaha unayoiingiza kwa muislamu..

صحيح الترغيب

Ukijua ubora wa jambo hili la kuingiza furaha katika moyo wa muislamu basi linganisha na hali waliyokuwa nayo baadhi ya waislamu wa zama hizi ambao wao jambo linalopendeza zaidi kwao ni kuingiza huzuni kwa mislamu au muumini !, unaweza ukamkuta muislamu yeye furaha yake ni pale anapomuona muislamu mwenzake amekosa raha !

إنا لله وإنا إليه راجعون ، لقد صدق الشاعر القائل :

إلى الله نشكو غربة الدين والهدى**وفقدانه من بين من راح أو غدا

فعاد غريبا مثل ما كان قد بدا**على الدين فليبكي ذوو العلم والهدى

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo mbili 7, 1443H ≈ Jun 7, 2022M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *