KUJIANDAA NA RAMADHANI

☞ Kujiandaa na ramadhani huanza sasa (kwani mwezi wa) Rajabu unatoweka kama upepo

قال أبو بكر الوراق البلخي – رحمه الله –

Amesema Abubakari Alwarraaq Al-bal-khiy-Allah amrahamu –

شهر رجب شهر للزرع، وشعبان شهر السقي للزرع

Mwezi wa Rajabu ni mwezi wa kupanda,
na (mwezi wa) Shabani ni mwezi wa kunywesheleza mazao,

ورمضان شهر حصاد الزرع،

Na (mwezi wa) Ramadhani ni mwezi wa kuvuna mazao,

وعنه قال: مثل شهر رجب مثل الريح

Na kutoka kwake (Al-warraaq) amesema:

Mfano wa mwezi wa Rajabu ni mfano wa upepo (unaondoka kwa kasi),

ومثل شعبان مثل الغيم، ومثل رمضان مثل القطر

Na mfano wa (mwezi wa) Shabani ni mfano wa wingu (linavyotoweka),
na mfano wa (mwezi wa) Ramadhani ni mfano wa tone (masiku machache),

وقال بعضهم: السنة مثل الشجرة:

Na wamesema baadhi yao:

Mwaka ni mfano wa mti,

وشهر رجب أيام توريقها،

Na mwezi wa Rajab ni siku za kuchipua kwake majani,

وشعبان أيام تفريعها، ورمضان أيام قطفها

Na (mwezi wa) Shabani ni siku za kutoa kwake matawi,
na (mwezi wa) Ramadhani ni siku za kuyachuma (matunda),

والمؤمنون قطافها،

Na waumini (waislamu) ndiyo wachumaji wake,

جدير بمن سود صحيفته بالذنوب،

Inaendana (zaidi) kwa yule aliyelitia weusi (aliyelichafua) daftari lake kwa madhambi,

أن يبيضها بالتوبة في هذا الشهر،

Alitie weupe (alisafishe) kwa kuleta toba katika mwezi huu,

وبمن ضيع عمره في البطالة،

Na kwa yule aliyeupoteza umri wake kwa kubweteka,

أن يغتنم فيه ما بقي من العمر.

Atumie fursa ndani ya (mwezi) huo kwa ule umri (wake) uliobaki.

📚 لطائف المعارف لابن رجب (ص ١٢)

Maelezo :

Ewe Allah tufikishe Ramadhani, na utubariki ndani yake na tupe msaada juu ya funga yake na kisimamo chake.

Mpitiaji : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo kumi 8, 1443H ≈ Feb 9, 2022M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *