قال ابن القيم – رحمه الله:
Amesema Ibn l-Qayyim – Allah amrahamu:
إذا أراد الله بعبدٍ خيراً: سلبه رؤية أعماله الحسنه من قلبه
Pindi Allah atakapomtakia kheri mja wake: humuondolea (ile hali ya) kuyaona matendo yake mema moyoni mwake,
والإخبار بها من لسانه،
Na (humzuia) kuyaelezea kwa ulimi wake,
وشغله برؤية ذنبه،
Na humshughulisha na kuyaona madhambi yake,
فلا يزال نصب عينيه حتى يدخل الجنة.
Basi (haya madhambi) huendelea kuwa mbele ya macho yake mpaka akaingia peponi.
📚 طريق الهجرتين (١٧٢)
[ Twariiqu l-hijratain (172) ]
Maelezo kutoka kwa Mfasiri – Allah amuhifadhi
Hii ndiyo sifa ya muumini, siku zote huidhania vibaya nafsi yake na kosa alilolifanya siku huliona kanakwamba lipo mbele yake limemganda, na huleta toba kwa kosa hilo, na hii ni dalili kuwa huyu muumini anaitambua nafsi yake kwa sababu mwenye kuidhania nafsi yake vizuri ni katika watu wajinga! kwa sababu mwenye kuidhania nafsi yake vizuri hujizuia na kuipekua nafsi yake na mabaya huyaona mema na kasoro huziona kuwa ni ukamilifu.
Tanbihi:
Maana ya kuidhania vibaya nafsi ni kuituhumu nafsi na wala si kumtuhumu Allah bali ni kuituhumu nafsi kuwa inamapungufu na aamiliane na nafsi yake muamala huu ili aizuie na tabia ya kujiona na kujigamba, lakini hilo lisimpelekee kumdhania Allah vibaya na wala lisimpelekee kukata tamaa na rehma za Allah, lakini anatakiwa muislamu ajitahidi katika kufanya ibada pamoja na kuituhumu nafsi yake na matendo yake hajui kuwa matendo yake yamekubaliwa au hayajakubaliwa kwa sababu Allah anasema:
{إنما يتقبل الله من المتقين }
{ Hakika si vinginevyo Allah huwakubalia wacha mungu }.
Muumini siku zote hujiona mpungufu na anapofanya dhambi hata kama ndogo huiona ni kubwa kama alivyoeleza Ibn Masud – Allah amridhie,
قال عبد الله بن مسعود – رضي الله عنه –
Amesema Abdullah bin Masud – Allah amridhie –
إنَّ المُؤْمِنَ يَرَى ذُنُوبَهُ كَأنَّهُ قاعِدٌ تَحْتَ جَبَلٍ يَخافُ أنْ يَقَعَ عليه،
Muumini huyaona madhambi yake kana kwamba yeye ameketi chini ya mlima anahofu ya kumporomokea,
وإنَّ الفاجِرَ يَرَى ذُنُوبَهُ كَذُبابٍ مَرَّ علَى أنْفِهِ فقالَ به هَكَذا،
Na bila shaka muovu huyaona madhambi yake kama inzi aliyepita juu ya pua yake akamfanya hivi (akamfukuza),
قالَ أبو شِهابٍ: بيَدِهِ فَوْقَ أنْفِهِ ..
Akafanya (akaashiria) abuu Shihab kwa mkono wake juu ya pua yake ..
📚 صحيح البخاري الصفحة أو الرقم (٦٣٠٨)
[ Sahih l-Bukhariy ukurasa au namba (6308) ].
Pia muumini huwa hana tabia ya kutaja mema aliyoyafanya ila kukiwa na maslahi katika kutaja hayo mema, na wala hayawazi moyoni mwake bali huyaona si chochote mbele ya Allah na huyaona makosa yake yapo mbele ya macho yake na hudumu na hali hii mpaka ikawa ndiyo sababu ya kuingia peponi.
Mfasiri : Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Toleo la pili : Mfungo nane 16, 1443H ≈ Dec 20, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•