🌸 والمرأة تخضع لزوجها بالقول فتسلك طريقها لقلبه
ولذلك نهى الإسلام أن تكلم المرأة الأجنبي بضعف وخضوع بالقول:
Mwanamke humlegezea sauti mumewe kwa mazungumzo ,na hupitia njia yake (hiyo) kwa kuufikia moyo wake na kwaajili hiyo uislamu umemkataza mwanamke kumzungumzisha mwanamume wa kando kwa unyonge na kulegeza sauti:
{ يَٰنِسَآءَ ٱلنَّبِىِّ لَسْتُنَّ كَأَحَدٍۢ مِّنَ ٱلنِّسَآءِ ۚ إِنِ ٱتَّقَيْتُنَّ فَلَا تَخْضَعْنَ بِٱلْقَوْلِ فَيَطْمَعَ ٱلَّذِى فِى قَلْبِهِۦ مَرَضٌ وَقُلْنَ قَوْلًا مَّعْرُوفًا }
{ Enyi wake wa Nabii! Nyinyi si kama yeyote katika wanawake wengine.Kama mnamcha Allah basi msilegeze sauti akatamani mwenye maradhi katika moyo wake. Na semeni maneno mazuri }
الأحزاب (٣٢).
ومفهوم المخالفة أن كلام المرأة مع زوجها يكون بالخضوع في القول
Na ufahamu wa kinyume kuwa : Mazungumzo ya mwanamke na mumewe huwa kwa kulegeza sauti
🌸 والمرأة ذات الحظوة عند زوجها ، والتي تصل إلى ما تريده منه ، إنما تصل إليه بضعفها لا بقوتها
Na mwanamke mwenye daraja /cheo kwa mumewe, na yule (anayeweza) kukifikia kile anachokitaka kutoka kwa huyo (mumewe), na hakika si vinginevyo (mwanamke) humfikia (mumewe) kwa kutumia unyonge wake na wala si kwa kutumia nguvu zake .
🌸 وتتسلل عادة إلي قلبه بضعفها لا بشراستها
Na kwa kawaida (mwanamke) huingia ndani ya moyo (wa mumewe) kwa unyonge wake na wala si kwa ukali wake
🌸. ولذلك تمدح بصبرها ، وسكوتها عن رد الإساءة ، وعدم مهاجمتها لزوجها
Na kwa ajili hiyo (mwanamke) husifiwa kwa kusubiri kwake na kunyamaza kwake kwa kuacha kurudisha ubaya na kumtomshambulia mumewe.
تمدح بحيائها ،وخوفها وبخلها .
🌸حتى قالوا عن هذه الصفات:
(Mwanamke) husifiwa kwa aibu yake na hofu yake na ubakhili wake ,mpaka wakasema kuhusu hizi sifa :
أنها مدح في المرأة وذم في الرجل ! وكل ما تمدح فيه هو من ضعفها .
Kwamba (tabia) hizo ni sifa mzuri kwa mwanamke na ni sifa mbaya kwa mwanamume, na kila (sifa) anayosifiwa (mwanamke) basi hiyo ni katika unyonge wake
.
المصدر: الصفحة الرسمية لموقع الشيخ محمد بازمول حفظه الله
Maelezo ya mfasiri:
Katika tabia ya mwanamke mwema ni kumnyenyekea mumewe na kumlegezea sauti pindi anapozungumza naye, kitendo cha kukatazwa kuwalegezea sauti wanamume wa kando ina maana amlegezee mumewe ! , na pia mwanamke anatakiwa ajue kuwa hawezi kukipata kile anachokitaka kutoka kwa mumewe kwa kutumia nguvu na ukali bali atavipata vitokavyo kwa mumewe kwa unyonge wake na unyenyekevu wake kwa mumewe na mwanamke akiwa hivyo basi atauteka moyo wa mumewe ! .Na mwanamke husifiwa kwa tabia yake ya uvumilivu na kukaa kwake kimya kwa kutorudisha majibu mabaya pindi anapokerwa na mumewe , na kutomshambulia kwake mumewe kwa maneno ..na pia mwanamke husifiwa kwa sifa yake ya kuwa na aibu sifa ambayo ni pambo la mwanamke ,na sifa ya hofu yaani kumuogopa Allah ,na sifa ya ubahili kwa sababu sifa hii itamfanya azitunze mali zake na mali za mumewe na hatotoa isipokuwa kwa kadri ya haja na hatofanya uharibifu katika matumizi, na katika hizi kuna sifa ambazo mwanamke akiwa nazo husifiwa na akiwa nazo mwanamume husemwa vibaya!kama vile sifa ya ubahili , Kwa kifupi kila sifa ambayo mwanamke husifiwa nayo ni katika udhaifu na unyonge wake mfano: Huruma wa kupita kiasi, ulaini n.k ,sifa hizi ni katika udhaifu wa mwanamke lakini ni sifa mzuri kwake .
Inaendelea..Allah akitaka
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo tisa 14, 1443H ≈ Jan 17, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•