🌸. فجمالك أيتها المسلمة هو في الضعف والخضوع لزوجك
لا في سلاطتك ومواجهته بقوة ، أو بصولة ..
Basi urembo wako ewe mwanamke wa kiislamu upo katika unyonge/udhaifu (ulionao) na kumnyenyekea kwako mumeo na wala (haupo) katika urefu wa ulimi wako na (haupo katika) kumuelekea kwako (mumeo) kwa nguvu na kwa mabavu .
قد تربحين بهذه الأخلاق جولة ، لكن جزما ستخسرين جولات أخرى !
Huwenda ukapata faida mara moja lakini bila shaka utakuja kupata hasara mara nyingine nyingi
🌸. ولا خضوعك وضعفك مع الأجانب ، فإن هذا باب شر ، عند من في قلبه مرض ، ولا أحد يأمن على نفسه !
Na wala (urembo wako) haupo katika kulegeza kwako (sauti) na (kuwa) dhaifu kwako (unapozungumza) na wanaume wa kando ,bila shaka huku ni (kufungua) mlango wa shari kwa yule ambaye katika moyo wake kuna maradhi, na wala hakuna yeyote anayeipa amani nafsi yake (juu ya maasi) !
🌸
والأنثى الحقيقية هي التي تتمنى أن يرزقها الله زوجا يحتوي ضعفها لا أن تخالفه وتظهر له دائما انها قوية ولا تحتاجه
Na mwanamke wa kweli ni yule ambaye anatamani Allah amruzuku mume atakayeukusanya unyonge wake, si kwenda kinyume naye na kumdhihirishia siku zote kuwa yeye ana nguvu na wala hamuihitajii huyo (mume)
و هي لا تعلم أنها بهذا الفعل تدفعه عن البحث عمن تُشعره وتحسسه بأنها بحاجة إليه وتظهر ضعفها له
Na wala yeye hajui kuwa yeye kwa vitendo vyake hivi humsukuma (mumewe) kumtafuta yule atakayempa hisia na akamzingatia kuwa ana haja naye na kumdhihirishia unyonge wake yeye
فجمالك أيتها الزوجة هو في ضعفك وخضوعك لزوجك
Basi urembo wako ewe mke upo katika unyonge wako na kumnyenyekea kwako mumeo/kumlegezea sauti.
.
الصفحة الرسمية للشيخ محمد بازمول حفظه الله
Maelezo ya mfasiri:
Urembo wa mwanamke haupo katika kurefusha ulimi wake na kuamiliana na mumewe kwa kutumia nguvu na mabavu na mwanamke akiwa na tabia hizi basi matokeo yake ni mabaya .l
Na mwanamke mwema halegezi sauti yake mbele ya wanaume wa kando kwa sababu kufanya hivyo ni kufungua mlango wa kufanyika machafu kwa wale wanaume wenye maradhi katika nyoyo zao, na wala haitakiwi mwanamke kuiamini nafsi yake kuwa yeye hawezi akaingia katika maovu kwa kulegeza kwake sauti kwa sababu mtu hatakiwi kuiaminisha nafsi yake na maovu.
Mwanamke mwenye sifa za kike ni yule anayemuomba Allah ampe mume ambaye atakayemtunza kwa sababu ya udhaifu wake na unyonge wake ,na wala haendi kinyume na amri za mumewe maadamu si za kumuasi Allah, na wala hamdhihirishii mumewe kuwa yeye ana nguvu na wala hamuhitajii mumewe na anaweza kuishi bila yeye ! .
Na mwanamke anatakiwa atambue kuwa akimfanyia hivi mumewe basi huyo mume atamtafuta mwanamke ambaye atamfanya ahisi kuwa yeye ni kidume na mwanamke atakayemdhihirishia kuwa ana haja na yeye na kumdhihirishia kuwa yeye (huyo mwanamke) ni dhaifu na mnyonge.
Ewe mke tambua kuwa uzuri wako unazidi kila unapodhihirisha unyonge na udhaifu wako kwa mumeo na ukamnyenyekea na kumlegezea sauti
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo tisa 15, 1443H ≈ Jan 18, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•