https://t.me/fawaidussalafiyatz
Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiya.net
KUSHIKAMANA NA TABIA YA UKWELI NI KAMA KUBEBA MILIMA JUU YA KICHWA !
🔺 قال ابن القيم رحمه الله:
▪️فحمل الصدق كحمل الجبال الرواسي. لا يطيقه إلا أصحاب العزائم. فهم يتقلبون تحته تقلب الحامل بحمله الثقيل،
Amesema ibn l-Qayyim- Allah amrahamu-:
Kuubeba ukweli ni kama kuibeba milima mikubwa iliyokita katika ardhi ,hawaliwezi hilo isipokuwa wenye maazimio basi (watu) hao wanajigeuza geuza chini ya huo (ukweli) kama anavyojigeuza mliyebeba (mzigo) mzito,
⏪ والرياء والكذب خفيف كالريشة لا يجد له صاحبه ثقلا البتة. فهو حامل له في أي موضع اتفق، بلا تعب ولا مشقة ولا كلفة. فهو لا يتقلب تحت حمله ولا يجد ثقله.
Na kujionesha na uwongo ni kwepesi kama nyoya mwenye (tabia) hiyo haoni uzito kwa hali yoyote .Basi huyo (mwenye tabia hii) ni mwenye kuubeba huo (uwongo) katika sehemu yoyote itakayoafikiana (na huo uwongo) ,bila tabu wala mashaka wala uzito , basi huyo (mwenye tabia hii) hajigeuzi geuzi chini ya mzigo wa huo (uwongo) na wala hapati uzito
📚 مدارج السالكين ٢\٢٦٤.
Maelezo ya muandaaji:
Uislamu umeamrisha ukweli na umehimiza ukweli katika kila muamala anaoufanya muislamu ,na dalili ni nyingi katika hizo ni kauli yake Allah – :
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ وَكُونُوا مَعَ الصَّادِقِينَ
Enyi mulioamini mcheni Allah ; na kuweni pamoja na wakweli .
التوبة: ١١٩.
Bila shaka ukiwa mkweli na ukalazimiana na ukweli utaokoka na yenye kuangamiza .
Na mtu akiwa mkweli basi ajue kuwa huo ukweli wake utamnufaisha siku ya kiama ,siku ambayo wale waongo watafedheheshwa kwa kuzibwa vinywa vyao na kutamkishwa viungo vyao .
Anasema Allah- aliyetukuka- pale alipotaja malipo ya kweli:
قَالَ اللَّهُ هَذَا يَوْمُ يَنْفَعُ الصَّادِقِينَ صِدْقُهُمْ لَهُمْ جَنَّاتٌ تَجْرِي مِنْ تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ ذَلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ
{Atasema Allah : “Hii ndiyo Siku ambayo wakweli utawanufaisha ukweli wao . Wao watapata pepo zipitazo chini yake mito .Humo watakaa milele .Allah amewaridhia ;nao watamridhia .Na huko ndiko kufaulu kukubwa .
المائدة: ١١٩ .
Ufafanuzi:
Hizi ni miongoni mwa fadhila za ukweli na matunda yake lakini huo ukweli kama alivyoeleza ibn l-Qayyim- Allah amrahamu- sifa ya ukweli ni kama kuyabeba majabali makubwa yaliyoenda chini kwa kina kirefu na bila shaka mwenye kubeba kitu kizito hupata shida na hujigeuza geuza huku na huko kutokana na uzito wa mzigo na hivi ndiyo tabia ya ukweli ilivyokuwa mzito !hawawezi kushikamana na tabia hii isipokuwa wale wenye maazimio makubwa !.
Ama tabia ya uwongo ni kama nyoya tu ambalo unaweza ukalipuliza kidogo likaruka mbali, huu ndio mfano wa uwongo hauna shida wala uzito mtu mwongo muda wowote anaweza kuongopa kwa sababu uwongo ni rahisi na mwepesi mno hauna mashaka wala uzito .
Tunamuomba Allah atukinge na tabia hii ya uwongo ambayo ni katika tabia za wanafiki .
Muandaaji: fawaidusalafiya.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiya.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Dhul-Qaadah 6, 1442H ≈ June 15, 2021M.
#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•