Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiya.net
الاهتمام بتطهير القلوب من السلفية
KUTILIA UMUHIMU KUZITWAHARISHA NYOYO NI KATIKA USALAFI
قــال الحافظ ابن رجب – رحمه الله:-
AMESEMA AL-HAFIDHI IBN RAJAB – ALLAH AMRAHAMU-
الاشتغال بتطهير القلوب أفضل،
من الاستكثار من الصوم والصلاة مع غش القلوب.
KUJISHUGHULISHA NA KUZITWAHARISHA NYOYO NI BORA ZAIDI .
KULIKO KUKITHIRISHA (KUZIDISHA) KUFUNGA NA KUSWALI PAMOJA NA NYOYO KUWA NA HADAA”
المصدر:
📚 لطائف المعارف (صـ ٤٢٧ )
[ Latwaif l-maarif (ukurasa ٤٢٧) ]
UFAFANUZI WA MTARJUMU -ALLAH AMHIFADHI NA AMSTIRI- : ✍🏾
Tunamuomba Allah hifadhi na thabati, ni mtihani mkubwa huu! kuna baadhi ya watu wapo hivi ukiwaona wamejipamba kwa muonekano wa sunnah lakini nyoyo zao zimejaa hadaa, chuki,khiyana, na husda! Na hili utaliona linadhihiri katika vitendo vyao, kuna wale wanao kula pesa za watu, wanawapa majukumu ya kazi watu fulani na pesa wanakula wao!
ukiwaona wana ndevu nguo zao ni nusu ugoko lakini nyoyo zao ni chafu sikusudii kuisema vibaya suna lakini hawa wanaiabisha suna na muislamu lazima ujue kuwa sio kila anaye jipamba na Sunnah ya kimuonekano anakuwa mtu wa sunnah yaani salafiy! hapana, bali kuna watu wana ndevu na nguo zao ni fupi, na wanaweza wakawa wanapiga vita baadhi ya bidaa lakini wakawa si watu wa sunnah bali ni watu wa vikundi vikundi na mahizb ambao ni maadui wakubwa wa dawa ya salafiyyah,watu waache kuwa na mafundo na chuki kwa waislamu wenzao !
Wamuogope Allah watu wajue dunia ni ya kupita, inafikia watu wanawapiga picha wanafunzi na vitabu vilivyotolewa waqfu kisha wanavikusanya!! uovu huu na hadaa, unyamaa huu hata mimi nilifanyiwa nilipokuwa mwanafunzi !!
Ndugu zangu tutakase nyoyo zetu, mpaka uwe muonekano wetu na nyoyo zetu ziwe sawa sawa
viongozi wa mataasisi mbali mbali wenye tabia hii tambueni kuwa mali mtaziacha Duniani.
Muandaaji: fawaidusalafiya.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiya.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: January 11, 2018 , na ikahakikiwa upya na kurushwa tena Shawwal 4, 1442H ≈ May 16, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•