🎙 أخذ حذيفة بن اليمان- رضي الله عنه- حجرين فوضع أحدهما على الآخر ثم قال لأصحابه: «هل ترون ما بين هذين الحجرين من نور؟»
قالوا: يا أبا عبد الله ما نرى ما بينهما من النور إلا قليلا.
قال: «والذي نفسي بيده لتظهرن البدع حتى لا يرى من الحق إلا قدر ما بين هذين الحجرين من النور,والله لتفشون البدع حتى إذا ترك منها شيئ قالوا: تركت السنة
(Siku moja) Hudhaifah bin l-yaman-Allah amridhie-alichukua mawe mawili (na) akaliweka (jiwe) mojawapo juu ya jingine kisha akawaambia watu wake:
Je munaona nuru iliyopo baina ya haya mawe mawili?
wakasema(kwa kujibu):
Ewe Abu-Abdullah! hatuoni baina ya mawe mawili katika nuru ila kidogo.
Akasema (Hudhaifah):
«Naapa kwa yule ambaye nafsi yangu ipo mkononi mwake zinadhihiri (zitadhihiri)bidaa mpaka haki haitoonekana ila kadri ya nuru (iliyopo) baina ya mawe haya mawili, naapa kwa Allah zitaenea bida’a (zitaenea) mpaka (itafikia kipindi) zikiachwa miongoni mwa (bida’a) (watu) watasema: (eeh!) Imeachwa sunnah!
📚 MAREJEO:⇣
الإعتصام للشاطبي( ص 61 )
[ Al-i’itisam, cha Asshatibiy,
ukurasa 61 ]
Mfasiri:fawaidusalafiya.net
*FAIDA:* 🎙
Maneno haya ya Hudhaifa yanachukua hukumu ya maneno ya mtume-swala na salamu zimwendee – kwa sababu ni katika mambo ya ghaibu hayajulikani isipokuwa kwa wahy.