Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net
إجزاء الأضحية عن الوالد وأولاده المتزوجين.
Kutosheleza (kichinjwa kimoja) cha udh’hiyah kwa mzazi na wanaye waliooa.
سئل الشيخ العباد – حفظه الله –
Aliulizwa Sheikh Al-Abbad – Allah amuhifadhi
هل تجزئ الأضحية عن العائلة التي يكون فيها أكثر من أسرة واحدة، أي: أن الوالد له أبناء متزوجون ولهم أبناء؟
====================
Je, kinatosheleza (kichinjwa) kimoja cha udh’hiyah kwa mkusanyiko wa ndugu ambao ndani yake kuna familia zaidi ya moja,
Yaani: Kwamba mzazi ana watoto waliooa na hao (watoto) wana watoto?
الجواب:
Jawabu:
إذا كانوا في بيت واحد فإنها تجزئ عنهم كلهم،
Wakiwa katika nyumba moja basi (kichinjwa) hicho kitawatosheleza wote,
وذلك إذا كانوا في بيت واحد وطعامهم واحد ومسكنهم واحد،
na hilo ni pindi wakiwa katika nyumba moja na chakula chao ni kimoja na makazi yao ni ma moja,
أما إن كان كل واحد مستقلاً في بيته وعائلته فكل واحد يذبح ذبيحة.
ama kama akiwa kila mmoja amejitenga katika nyumba, basi kila mmoja atachinja kichinjwa (chake).
📚 شرح سنن أبي داود للعباد (٣٣١/ ٣٠)
Maelezo ya mfasiri:
Familia inayokaa nyumba moja anawatosha mbuzi/kondoo mmoja tu , kama hili swali aliloulizwa sheikh- Allah amuhifadhi- mtu ambaye anaishi na wanaye na wajukuu zake ,na wanashirikiana katika chakula n.k ,katika hali hii mbuzi mmoja au kondoo mmoja anawatosha ,na wakiamua kuchinja zaidi ya mmoja basi ni bora zaidi.
Na udh’hiya katika madhehebu (ya kishafii) ni suna ya kutoshelezana katika mkusanyiko wa watu akitekeleza mmoja wao ,basi yatosha kama vile familia moja inayoishi katika nyumba moja mfano wa hili swali alilojibu sheikh.
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Iliandaliwa: 1 Dhul-Hijjah 1441H = 22/July /2020M ikarudiwa tena : 2/Dhul-Hijjah /1442H =Jul 12,2021M
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•