سئل أحد السلف :
Aliulizwa mmoja wa (wema) waliopita
“متى يكون العبد مخلصاً ؟
Ni wakati gani mja atakuwa ni mwenye kufanya matendo yake kwa ajili ya Allah ?
فقال: إذا صار خُلُقه كخُلقِ الرّضيع لا يُبالي من مدحهُ أو ذمّه”.
Basi akajibu (hivi):
“ (Ni pale) itakapokuwa tabia yake ni kama tabia ya kitoto kinachonyonya (ambaye yeye) hajali yule aliyemsifu au aliyemponda”
📗 تنبيه المغترين (٧٨)
Maelezo ya mfasiri:
Hivi ndiyo inavyokuwa tabia ya mwenye kufanya amali zake kwa ajili ya kutafuta radhi za Allah -aliyetukuka- yeye huwa hajali kama watu wanamsifu au wanamsema vibaya, kwa sababu yeye lengo lake ni kumridhisha Allah -aliyetukuka- na si kuwaridhisha watu,na bila shaka kusifika na tabia hii ni jambo gumu kwa maana kufanya matendo kwa ajili ya Allah pekee ni jambo zito kwa sababu nafsi ya mwanadamu inapenda kusifiwa na pindi inaposemwa vibaya hunyongea!.
Kwa ajili ya uzito wa jambo hili la kufanya amali kwa ajili ya Allah mmoja katika wema waliopita amezungumza maneno ambayo yanastahiki kuenezwa, na haswa kwa wale wenye kujihusisha na elimu ya kisheria :
قال سفيان الثوري -رحمه الله-
Amesema Sufian Athauriy -Allah amrahamu-:
«مَا عَالَجْتُ شَيْئًا أَشَدَّ عَلَيَّ مِنْ نِيَتيِ ، إنَّها تَقَلَّبُ عَلَيَّ »
“Sijapatapo kuamiliana na kitu chochote kilichokuwa kigumu zaidi juu yangu kuliko nia yangu, hakika hiyo (nia) hunibadilikia badilikia ”
الجامع لأخلاق الراوي وآداب السامع للخطيب البغدادي (2/288).
قال الشيخ عبد الرزاق البدر -حفظه الله – معلقا على هذا الكلام :
Amesema sheikh Abdul-Rrazzaq Al-badr-Allah amuhifadhi- hali ya kuyawekea maelezo mafupi haya maneno:
كثرة تقلب النية سببه كثرة ما يغشى القلب ويهجم عليه
Wingi wa kubadilika badilika nia sababu yake ni wingi wa vile vinavyoufunika moyo na kuuvamia,
من الصوارف والصواد،
katika vile vyenye kuutoa moyo kutika (mambo mema) ,na yale yenye kuuzuia moyo kufanya mema
مما يتطلب دوام ملاحظة وعناية وإلا عطب وهلك، والله الحافظ.
(Mambo) ambayo yanamtaka (muislamu) awe ni mwenye kudumu kuukagua (moyo) na kuutilia umuhimu na kama hakufanya hivyo atateketea na kuangamia, na Allah pekee ndiye mwenye kuhifadhi.
Nyongeza ya mfasiri:
Ikiwa wema waliopita wanasema kuwa walipata shida sana katika kupambana na nafsi zao na kuzilazimisha ili zidumu na ile hali ya kufanya ibada kwa ajili ya Allah pekee bila shaka sisi watu wa zama hizi tuna haki zaidi ya kuzipinda nafsi zetu ,na kama alivyosema sheikh Abdul-Rrazzaq -Allah amuhifadhi- kuwa vishawishi ni vingi vyenye kuufunika moyo kama vile : Kupenda kujulikana,kujionesha,kupenda dunia,n.k , na akasema kuwa mwenye uwezo wa kukuhifadhi ni Allah pekee, kwa maana inawajibika kwa muislamu amuelekee Allah kwa kumuomba hifadhi, na haswa katika zama hizi ambazo kumekithiri ndani yake vitu vingi vyenye kuharibu ikhlasi ya mtu kama vile mitandao ya kijamii ambayo shetani huitumia pia kama mitego ya kuwanasa watu na kuwaingiza katika maovu mbalimbali na kwa wale walinganiaji Shetani hufanya kila juhudi ya kuwaingiza katika ushirikana mdogo wa kufanya matendo ili watu wawaone au kutafuta wafuasi wengi au kukusanya kundi kubwa la watu wanaowafuatilia (Followers) !.
•┈┈┈┈••✦✿✦•
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa : Mfungo mosi 16 , 1445H =Apr 25, 2024M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•