Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net
KUWAFARIJI WAUMINI .
▫️قال ابن القيم رحمه الله:
“المواساة للمؤمنين أنواع:
Amesema ibn l-Qayyim- Allah amrahamu- : Kuwafariji waumini kuna aina mbalimbali:
•مواساة بالمال ومواساة بالجاه، ومواساة بالبدن،
Kuwafariji (waumini) kwa mali na kuwafariji kwa cheo ,na kuwafariji kwa mwili,
ومواساة بالنصيحة والإرشاد، مواساة بالدعاء والاستغفار، ومواساة بالتوجع لهم.
Na kuwafariji kwa nasaha, na kuwapa muongozo,na kuwafariji kwa kuwaombea dua na, kuwatakia msamaha na kuwafariji kwa kuumia (moyoni) kwa ajili yao .
•وعلى قدر الإيمان تكون هذه المواساة، فكلما ضعف الإيمان ضعفت المواساة، وكلما قوي قويت،
Na kwa kadri ya imani huwepo (hali) hii ya kufariji ,basi kila imani inapokuwa dhaifu hudhoofika (huku) kufariji,na kila (imani) inapokuwa na nguvu (kufariji) huwa na nguvu,
وكان صلى الله عليه وسلم أعظم الناس مواساة لأصحابه بذلك كله،
Na Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie- ni mtu mwenye kuwafariji mno maswahaba wake kwa (aina) zote za kuwafariji,
فلأتباعه من المواساة بحسب اتباعهم له”.
Basi wafuasi wake wanasifa hii ya kufariji kwa kadri ya kumfuata kwao huyo (Mtume).
📚 الفوائد (ص176-177
Maelezo ya mtarjumu:
Kuwafariji waislamu kuna aina mbalimbali:
1-Kuwafariji waumini wasiojiweza kwa kuwapa kama pesa na mali mbalimbali .
2- Kuwafariji kwa kuwasaidia kwa nafasi na cheo ulichokuwa nacho .
3 – Kuwafariji kwa kutumia nguvu zako kwa kufanya yale yanayotumia nguvu .
4- Kuwafariji kwa kuwapa nasaha mzuri na kuwapa muongozo katika yale yenye kuwanufaisha .
5- Kuwafariji kwa kuwaombea dua na kuwatakia msamaha na tena muislamu akilifanya hili kwa mwenzake bila ya kumuomba bila shaka hiyo ni ishara ya nguvu ya imani.
6- Kuwafariji waumini kwa kuhisi maumivu na huruma kwa hali waliyokuwa nayo kama kuvamiwa na adui,maradhi,dhiki n.k.
Kisha imam ibn l-Qayyim-Allah amrahamu- akaeleza kuwa hii tabia ya kuwafariji waumini na kuwaliwaza huwepo katika moyo kwa kadri ya imani yaani pindi imani inapokuwa dhaifu basi hupungua hali hii ya kuwafariji waumini na pindi imani inapokuwa na nguvu hukithirisha kuwafariji waumini.
Kisha sheikh akaeleza kuwa Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie- alikuwa ni mtu mwenye kuwafariji maswahaba wake kwa aina zote za kufariji , na wafuasi wa Mtume-swala na salamu za Allah zimfikie- yaani waislamu huwa na tabia hii ya kufariji kadri ya kumfuata kwao Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie- kwa maana mwenye kumfuata sana mtume huzidi kwake tabia ya kuwafariji waumini na anapokuwa na upungufu wa kumfuata Mtume pia hupungua kwake tabia ya kufariji.
Kuwafariji marafiki na kuwasaidia wanaostahiki kusaidiwa kwa kuwapa katika mali na vyakula na vinginevyo hilo linaingia katika kauli yake Allah-:
{ وَتَعَاوَنُوا عَلَى الْبِرِّ وَالتَّقْوَى وَلَا تَعَاوَنُوا عَلَى الْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ}
{Na saidianeni katika wema na ucha Mungu . Wala msisaidiane katika dhambi na uadui .
المائدة: ٢.
Mwisho:
Ikiwa kuwafariji waumini ni katika alama ya imani je kuwaingizia waumini au waislamu matatizo na misukosuko au kuacha kuwasaidia hali ya kuwa una uwezo wa kuwasaidia , bila shaka huo ni upungufu wa imani !
Mtarjumu: Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshaafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo sita 20, 1443H ≈ October 26, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•