KUWAGOMBANISHA WATU WANAOPENDANA NI KATIKA MADHAMBI MAKUBWA.

قال ابنُ عبدالبرّ المالكي رحمه الله:

Amesema ibn Abdil- Barr Al-Maalikiy- Allah amrahamu-:

«والتحريشُ بين البَهائِم مَكروه ، والتحريشُ بين الآدَمِيِّين حَوبٌ كبير ،

Kuchonganisha baina ya wanyama ni (jambo) linalochukiza na kuchonganisha baina ya wanadamu ni dhambi kubwa,

وأبغضُ الخلقِ إلى الله وأبعدهم من رسول ﷺ ؛ المشّاؤُون بالنمِيمَة ،
Na viumbe wenye kuchukiza zaidi kwa Allah, na waliokuwa mbali zaidi na Mtume wa Allah- swala na salamu za Allah zimfikie- ni wale wenye kutembea (huku na huku) kwa umbea,

المُفَرِّقُون بين الأحِبَّة ، المُلتَمِسُون لأهل البِرِّ العَثَرات!»

wenye kutenganisha baina ya waliopendana ,wenye kuwatafutia makosa watu wema “

الكافي في فقه أهل المدينة(١١٤٤/٢)

Maelezo ya mfasiri:

Haifai kuwachonganisha wanyama ili wapigane , na imamu Nnawawiy- Allah amrahamu- amesema kuwa ni haramu kwa hadithi iliyokuja kukataza hili pamoja na udhaifu uliyopo ndani yake – kwa sababu kufanya hivyo ni kuwaumiza wanyama na kuwachosha bila ya faida bali ni kwa ajili ya mchezo kama alivyosema Asshaukaniy- Allah amrahamu.

Ama kuwachonganisha watu na kuwagombanisha hiyo ni dhambi kubwa ,kama alivyosema Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie-:

” إنَّ أحبَّكم إليَّ أحاسنُكم أخلاقًا المُوطؤونَ أكنافًا الذين يألَفون ويؤلَفونَ

Hakika wanaopendeza zaidi kwangu wazuri wenu zaidi wa tabia, wepesi/walaini ambao hupata maliwazo (kwa watu) na watu hupata maliwazo kwao

وإنَّ أبغضَكم إليَّ المَشَّاؤونَ بالنَّميمةِ المُفرِّقونَ بين الأَحِبَّةِ المُلتمِسونَ للْبُراءِ العَنتَ

Na hakika wenye kuchukiza zaidi kwangu ni wenye kutembea kwa ajili ya umbea wenye kuwatenganisha baina ya wanaopendana,wenye kuwatafutia makosa wale waliokuwa mbali na makosa.

السلسلة الصحيحة ٢٥٠/٢

Ufafanuzi wa hadithi:

Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie- anaeleza kuwa miongoni mwa watu watakaokuwa karibu na yeye siku ya kiama peponi ni wale wenye tabia njema ,na watu wenye sifa ya wepesi na upole ambao huamiliana na waumini kwa upole na wepesi na tabia njema, huzoeana na watu na hufurahi na kutabasamu na huliwazika nao ,na watu pia hujiliwaza kwao na huwapenda.

Kisha akawataja miongoni mwa watu wenye kuchukiza zaidi kwake nao ni wambea watu ambao kazi yao ni kugombanisha baina ya watu huchukua maneno huku na kupeleka kule ili kuwagombanisha na kuwatenganisha, kawaida ya watu hawa hawapendi kuwaona watu wawili wakipendana , na pia watu wenye kupekua aibu za watu na kuziweka wazi kwa watu na kuwafedhehesha.

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo tisa 10, 1443H ≈ Jan 13, 2022M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *