Kwa mwenye kutaka kufungua hazina za Allah .

قال الشيخ صالح_الفوزان -حفظه الله-

Amesema shekh Saleh Alfauzan Allah- amuhifadhi-

‏الدُّعاء هو مفتاح خزائن الله جلّ وعلا،

Dua ni funguo za hazina za Allah- aliyetukuka na aliyekuwa juu-,

فإذا
‏أردتَ فتْحَ خزائن الله فأكثرْ من الدُّعاء.

basi pindi utakapotaka kufungua hazina za Allah kithirisha kuomba dua.

‏-شرح منظومة الآداب الشرعية (٥٣٠)

Maelezo ya mpitiaji:

Allah ndiye mwenye miliki ya kweli ya kila kitu na mwenye hazina ya kila heri kama riziki na vinginevyo ,kama ikiwa ni hivyo basi wakuelekewa ni yeye pekee ,na Allah yeye anapenda kuombwa ,na yule ambaye hamuombi Allah hata kidogo au akaacha kumuomba kwa kiburi tu au kwa kujiona kuwa yeye ametosheka basi mtu huyo yupo katika hatari kubwa kwa sababu Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie- amesema:

” إِنَّهُ مَنْ لَمْ يَسْأَلِ اللَّهَ يَغْضَبْ عَلَيْهِ“.

“ Hakika hali ilivyo, yule asiyemuomba Allah humkasirikia ”

رواه الترمذي ،والبخاري في الأدب المفرد .

Hii ni hadithi ambayo baadhi ya wanawavyuoni wanaona kuwa sanadi yake ni nzuri .

Namalizia kwa maneno ya mshairi pale aliposema :

“لاَ تَسْأَلَنَّ بُنَيَّ آدَمَ حَاجَةً

Usimuombe binadamu haja (yako).

وَسَلِ الَّذِي أَبوَابُه لاَ تُحْجَبُ

Na muombe yule ambaye milango yake haifungwi.

اللهُ يَغْضَبُ إِن تَرَكْتَ سُؤَالَهُ

Allah anakasirika kama ukiacha kumuomba .

وَبُنَيَّ آدَمَ حِينَ يُسْأَلُ يَغْضَبُ.”

Na mwanadamu pindi anapoombwa hukasirika .

Mfasiri : Ummu Muhammad .

Ameipitia : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy.

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo mosi 10, 1445H ≈ Apr 19, 2024M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz

       •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *