KWA NINI FUNGA YA ARAFAH INAFUTA MADHAMBI YA MIAKA 2 NA FUNGA YA A’SHURAA INAFUTA MADHAMBI YA MWAKA 1

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net

═════════ ❁ ❆

لماذا عاشوراء يكفر سنة ويوم عرفة يكفر سنتين؟

KWANINI (FUNGA) YA ‘AASHURAA INAFUTA MADHAMBI YA MWAKA MMOJA NA (FUNGA) YA A’RAFA INAFUTA (MADHAMBI) YA MIAKA MIWILI?

🎙 قال العلامة ابن القيم- رحمه الله-:

AMESEMA MWANACHUONI MKUBWA IBNUL QAYYIM :(ALLAH AMRAHAMU)

الأول: أن يوم عرفة في شهر حرام, وقبله شهر حرام, وبعده شهر حرام,بخلاف عاشوراء. الثاني: أن صوم يوم عرفة من خصائص شرعنا, بخلاف عاشوراء, فضوعف ببركات المصطفى.

La kwanza : Kwamba siku ya ‘Arafah (ipo) katika mwezi mtukufu na kabla yake (kuna) mwezi mtukufu na baada yake (kuna) mwezi mtukufu kinyume na (siku ya) ‘Aashuraa.

La pili: Kwamba funga ya siku ya ‘Arafah ni katika (mambo) makhsusi ya sheria yetu kinyume na (funga) ya ‘Aashuraa, basi kukaongezwa (malipo yake) kwa baraka za mteuliwa.

📚 REJEA:⇣

​بدائع الفوائد211/4​

[ Badaai’a l-fawaaid 4/211]

   UFAFANUZI: 🎙

“Kwa baraka za mteuliwa”

Anakusudia baraka za mtume wetu Muhammad -swala na salamu za Allah ziwe juu yake- kwani yeye amebarikiwa na hata maswahaba walikuwa wakitabaruku kwa vile vinavyotoka mwilini mwake kama jasho lake ,mate, nywele zake kwa sababu baraka yake Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie- ni baraka ya kidhati ,
kwa maana Allah ndiye aliyembariki Mtume wake na akaifanya kuwa ni baraka ya kidhati .

Na hili la kutafuta baraka kwa vile vilivyotoka katika mwili wa Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie- lilikuwa pindi alipokuwa hai au baada ya kufa ikiwa zile athari zake bado zipo kama nguo zake au nywele zake na vinginevyo na hii ni maalumu kwake tu yaani haifai kutabaruku kwa yeyote katika viumbe ila kwa mtume Muhammad-swala na salamu za Allah ziwe juu yake- na kwa mitume wengine katika uhai wao, ama baada ya kufa na kupotea athari zake haifai.

Na pia haifai kuomba dua kwa kusema “kwa baraka za Mtume wetu Muhammad” jambo hili ni haramu tena ni njia ya kuingia katika ushirikina na pia haifai kwenda kutabarruku katika kaburi lake na wala halikuthibiti hilo kutoka kwa maswahaba.

Ama baraka ya muislamu ni ile imani yake na matendo yake kwa maana kila muislamu ana baraka kwa ile imani aliyokuwa nayo na matendo mema ,lakini baraka zao si kama baraka za Mitume -Amani iwe juu yake- na wala haifai kutabarruku kwa yeyote isipokuwa kwa Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie- kwa ajili hii maswahaba hawakuwa wakitabaruku kwa Abuu Bakr na Omar Allah awaridhie-.

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Iliandaliwa: August 31,2017M , na ikarudiwa tena Dhul-hijjah 5, 1442H ≈ Jul 15, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *