KWA WALIOSHINDWA KUWAADABISHA WATOTO WAO !

كان من دعاء الْفُضَيْلِ بن عياض -رحمه الله- وهو يدعو لابنه “علي” وكان ولدًا مستهترًا طائشًا:

Zilikuwa miongoni mwa dua za Fudhail bin I’yadh-Allah amraham-na hali yeye akimuombea mwanaye (anayeitwa) Aliy na (huyo Aliy) alikuwa ni mtoto mwenye michezo mingi, (na hayuko) makini

﴿اللهم إني اجتهدت أن أؤدب عليا فلم أقدر على تأديبه فأدّبه لي﴾

{ Ewe Allah!hakika mimi nimejitahidi kumuadabisha Aliy lakini sikuweza kumuadabisha ,basi niadabishie}

فهداه الله تعالى بدعاء والده له.
Basi Allah-aliyetukuka- akamuongoza kwa sababu ya dua ya mzazi wake kwake.

يقول الذهبي عنه -رحمه الله-:

Anasema Addhahabiyy -Allah amrahamu-kuhusu huyo (mtoto Aliy):

“كان علي بن الفضيل من كبار الأولياء،

Alikuwa (huyo) Aliy bin Fudhail miongoni mwa vipenzi vya Allah,

وكان قانتا لله خاشعا وجلا ربانيا كبير الشأن”.

na alikuwa ni mwenye kumnyenyekea Allah ,mwenye kumuogopa Allah ,mwenye kumuabudu Mola Mlezi wa viumbe vyote, mwenye nafasi kubwa .

📚 سير أعلام النبلاء : ٧/ ٤٠٨

Maelezo ya mfasiri:

Kama umejitahidi kumuadabisha mwanao na ukashindwa basi muelekee Allah -aliyetukuka- kwa kumuomba akuadabishie huyo mwanao, na kama utamuomba Allah kwa ukweli basi Allah atajibu dua yako na mwanao atakuwa ni katika watu wema kama alivyokuwa mtoto huyu, na hata kama umejitahidi kumuadabisha na ukamuomba Allah dua amuadabishe lakini akawa hajabadilika basi tambua kuwa huo ni mtihani ambao Allah amekujaribu na katika hilo unamalipo kutoka kwa Allah.

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa:Rajabu 2, 1445H ≈ Ja 14, 2023M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz

       •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *