◾️ قال ابن القيم رحمه الله:
Amesema ibn l-Qayyim -Allah amrahamu-:
▫️يقرن استواءه على العرش بهذا الاسم كثيرا، كقوله تعالى:
(Allah) huambatanisha (sifa ya) kuwa kwake juu ya A’rshi na jina hili (la Arrahman) mara nyingi, kama vile kauli yake (Allah) aliyetukuka- :
﴿ ٱلرَّحْمَٰنُ عَلَى ٱلْعَرْشِ ٱسْتَوَىٰ ﴾
{ Mwingi wa Rehema ,aliyekuwepo juu ya A’rshi }
Surat-t’aha (5)
﴿ ثُمَّ اسْتَوَى عَلَى الْعَرْشِ الرَّحْمَنُ ﴾
{ Kisha akawa juu ya A’rshi ,Mwingi wa Rehema }
Surat al furqan 59
▫️فاستوى على عرشه باسم “الرحمن”، لأن العرش محيط بالمخلوقات قد وسعها،
Basi (Allah) yupo juu ya A’rshi yake kwa jina la “Mwingi wa Rehema ” kwa sababu A’rshi ni yenye kuvizunguka viumbe (vyote) na imevienea,
والرحمة محيطة بالخلق واسعة لهم،
Na rehema (ya Allah) ni yenye kuwazunguka viumbe na ni yenye kuwaenea
كما قال تعالى:
Kama alivyosema (Allah ) aliyetukuka:
﴿ ۖ وَرَحْمَتِي وَسِعَتْ كُلَّ شَيْءٍ ۚ ﴾
Na rehema yangu imekienea kila kitu .
Al aaraf (156)
فاستوى على أوسع المخلوقات بأوسع الصفات، فلذلك وسعت رحمته كل شيء.
Basi (Allah) akawa juu ya kiumbe kipana zaidi (kilichoenea zaidi) (ambacho ni A’rshi) kwa sifa iliyoenea zaidi (sifa ya rahma) basi kwa ajili hiyo ،rehema yake imeenea kila kitu .
📚 مدارج_السالكين (١/ ٥١).
Maezo ya mfasiri:
Sheikh -Allah amrahamu-anataja siri ya kuambatanishwa jina la Allah la “Arrahman” lenye maana ya mwingi wa Rehma na sifa ya Allah ya kuwa kwake juu ya A’rshi, akasema kuwa siri iliyopo katika hilo ni hii :
A’rshi ni kiumbe kikubwa zaidi kuliko vyote ambacho kimevizunguka viumbe vyote na kuvienea kwa sababu A’rshi ni paa la viumbe ,na pia rehma ya Allah imevizunguka viumbe vyote hapa duniani hata makafiri !hebu angalia neema mbalimbali ambazo viumbe huogelea ndani yake kama vile :Vyakula,vinywaji ,mavazi, na neema mbali mbali zinazoonekana na zisizoonekana ,na hizi neema zote ni katika athari ya rehma za Allah ,kwa hiyo Allah -aliyetukuka- akawa juu ya kiumbe kilichokuwa kipana zaidi na kuenea zaidi kwa sifa yake iliyoenea kila kitu .
Tanbih :
Tunaposema kuwa Allah yupo juu ya A’rshi tuna maana kuwa yupo juu hakika uwaji juu ambao unanasibiana na utukufu wake na kuamini kuwa Allah yupo juu ya A’rshi ni wajibu na kuuliza na kutafuta namna namna ni uzushi na haramu ,na Allah hafanani na chochote na tunathibitisha majina yake na sifa zake kama alivyojithibitishia mwenyewe na Mtume wake, na wala hatupingi ,na hatufananishi,na hatupindui maana .
Amesema ibn Taimiyyah Al-Hanbaliy -Allah amrahamu-katika beti zinazonasibishwa kwake :
هذا اعْتِقَـادُ الشَّافِعيِّ ومَالِكٍ
وَأَبِي حَنِيفَـَةَ ثُمَّ أَحْـمَدَ يُنْقَـلُ
Hii ndiyo itikadi ya Shafii na Maliki, na Abuu Hanifah kisha Ahmad hunukuliwa (kwake itikadi hii) .
فَإِنِ اتَّبَعْتَ سَبِيلَهُمْ فَمُوَفَّقٌ
وَإِنِ ابْتَدَعْتَ فَمَا عَلَيْكَ مُعَـوَّلُ
Kama utafuata njia yao basi (utakuwa) ni mwenye kuafikishwa,
Na kama utazusha basi (tambua kuwa) hauna pakutegemea .
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo sita 23, 1443H ≈ Oct 19, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•