قال الشيخ أحمد بن ناصر علوان المصري -حفظه الله -:
Amesema sheikh Ahmad bin Nasir ‘Al-wan Al-Masry -Allah amuhifadhi-:
كيف نرد على من يحاول النيل من النبي – صلى الله عليه وسلم- بالسب وما شابه ذلك ؟
Vipi tutamjibu yule anayejaribu kumtukana Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie – kwa kumtupia maneno machafu na mfano wa hayo ?
ندرس سيرته وندرسها ونعمل بها وننشرها للعالمين .
Tuisome sira yake /hisoria ya maisha yake, na tuifundishe, na tuifanyie kazi, na tuisambaze kwa walimwengu.
المصدر :
Maelezo ya mfasiri :
Bila shaka kuna umuhimu mkubwa bali ni wajibu kwetu sisi waislamu kuisoma Sirah yaani historia ya maisha yake Mtume wetu -swala na salamu ziwe juu yake -tokea kuzaliwa kwake mpaka kufa kwake na haswa katika wakati huu tuliokuwa nao.
Amesema sheikh Swaleh Al-‘uswaim -Allah amuhifadhi – :
وتتأكد العناية بالسيرة النبوية في مقامين :
Kunakokotezeka (uwajibu) wa kuitilia umuhimu sirah ya Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie -sehemu mbili :
أحدهما : غلبة الجهل بها وضياع علمها في الأمة
Moja wapo : Kuzidi ujinga wa kutoijua hiyo (sira) ,na kupotea elimu yake katika ummah.
والآخر : فشو قالة السوء من المنافقين والكافرين في الجناب النبوي .
Na (sehemu) nyingine : Kuenea maneno mabaya kutoka kwa Wanafiki na Makafiri kwa upande wa Mtume -swala na salamu zimfikie – .
المصدر : شرح الأرجوزة الميئية في ذكر حال أشرف البرية
Ufafanuzi :
Bila shaka katika kipindi tulichopo yote mawili aliyoyataja sheikh yapo :
1- Ujinga umeenea na kuzidi sehemu kubwa zaidi ya waislamu hawamfahamu Mtume wao -swala na salamu za Allah zimfikie – ukweli wa kumfahamu.
2- Matusi na kejeri yamekithiri juu ya Mtume wetu -swala na salamu za Allah zimfikie -haupiti muda isipokuwa tunasikia Makafiri wakimtusi Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie – .
Mkusanyaji na mfasiri: Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo pili 10, 1443H ≈ Jun 9, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•