Maana sahihi ya kuwafuata wema waliopita .

قال العلامة محمد بن صالح العثيمين ـ رحمه الله ـ :

Amesema mwanawachuoni mkubwa Muhammad bin Swaleh Al-Uthaimin- Allah amrahamu – :

((السلفية هي اتباع منهج النبي وأصحابه، لأنهم هم الذين سلفونا و تقدموا علينا، فاتباعهم هو السلفية،

Usalafi ni kufuata njia ya Mtume na maswahaba wake Kwa sababu wao ndiyo ambao wamepita kabla yetu na wametutangulia (katika dini) basi kuwafuata hao huo ndiyo usalafi

وأما اتخاذ السلفية كمنهج خاص ينفرد به الإنسان ويضلل من خالفه من المسلمين ولو كانوا على حق، فلا شك أن هذا خلاف السلفية))،

ama kuufanya usalafi kama njia maalumu mtu akajitenga nayo na (akawa) anamtia katika upotevu yule aliyeenda kinyume na yeye katika waislamu, hata kama hao (waislamu) walikuwa katika haki, basi hakuna shaka kwamba hivi ni kinyume na usalafi

وقال

Na (sheikh) akasema (tena) :

((لكن بعض من انتهج السلفية في عصرنا هذا صار يُضلل كل من خالفه ولو كان الحق معه،

Lakini baadhi ya wale waliofuata njia ya wema waliopita katika zama zetu hizi wamekuwa wakimtia katika upotevu kila aliyeenda kinyume na wao hata kama haki ipo pamoja na yeye

واتخذها بعضهم منهجاً حزبياً كمنهج الأحزاب الأخرى التي تنتسب إلى الإسلام))

Na wakaufanya baadhi yao huo (usalafi) kuwa ni njia ya kikundi kama vile njia ya makundi mengine ambayo yanajinasibisha na uislamu.

لقاء الباب المفتوح السؤال رقم (١٣٢٢).

(( فالسلفية بمعنى أن تكون حزباً خاصاً له مميزاته ويضلل أفراده سواهم فهؤلاء ليسوا من السلفية في شيء))

Usalafi kwa maana ya kuwa kikundi maalumu na kina (taratibu maalumu) zinazoupambanua, na watu wake wanawatia katika upotevu wasiokuwa wao,basi hawa (wenye sifa hizi) hawana sifa yoyote ya usalafi .

Maelezo ya mfasiri:

Maneno ya mwanawachuoni huyu yapo wazi kabisa katika kupinga vikali suala la kuufanya usalafi kuwa ni kikundi fulani ambacho kikawa kinawatia watu katika upotevu bila ya haki kwa madai ya kuwa wao ndiyo masalafi na wengine ni watu wa bidaa ,na tuelewane vizuri hapa shekhe hakupinga usalafi bali amepinga uhizbi ndani ya usalafi na bila shaka hili wameliingia baadhi ya ndugu zetu kwa kufuata matamanio ya nafsi zao au wengine kwa kufuata mkumbo kwa sababu ya ujinga wao, na mwisho tunasema hivi maneno ya sheikh yapo wazi kabisa katika kupinga jambo hili baya ambalo baadhi ya watu wamelifanya kuwa ndiyo njia ya wema waliopita! na kama utawaonesha maneno kama haya ya wanawachuoni huyapindua na kudai kuwa sheikh hakusudii hivyo! na hali ya kuwa maneno yapo wazi mno kuwa sheikh -Allah amrahamu-anawakusudia hawa wenye kuchupa mipaka katika kuwatoa watu katika sunnah na kuwaingiza katika bid’aa bila ya kutumia misingi ya kisheria kutokana na mwenendo wao huu mbaya waliokuwa nao na kuna watu ambao wamewakubali basi wakatengeneza kikundi na unaweza ukamsema kuwa mbona wenyewe wanasema kuwa hawajatengeneza kikundi ?

Jawabu :

لسان الحال أفصح من لسان المقال

“Lugha ya kimatendo inafahamika zaidi kuliko lugha ya kimaneno”,

maana yake ni kwamba kile kitendo cha kuwa na mfumo huu maalumu wa kuchupa mipaka kwa kuwatia watu katika upotevu kama alivyoeleza sheikh, basi huko ni kujianzishia kikundi hata kama haujazungumza kwa kinywa chako kuwa umeanzisha kikundi, na mbaya zaidi ni pale utapowaona watu hawa wakiwatoa watu katika sunnah na kuwaingiza katika bid’aa na hali wao wenyewe ukiwapekua hawaepukani nayo !.

Na mengine yanayoambatana na hayo ni dharau na kiburi walichokuwa nacho hata kwa wale waliowazidi katika elimu jambo ambalo linapelekea wanafunzi wao pia wakawa na tabia hiyo kama alivyosema mshairi:

إذا كان رَبُّ البيتِ بالدفِّ ضارباً

فشيمةُ أهلِ البيت كلِّهِمُ الرَّقصُ

Ikiwa mwenye nyumba ni mpiga ngoma , basi tabia ya watu wa nyumba (hiyo) wote (itakuwa ni) kucheza ngoma .

Tabia nyingine ni kitendo cha kunadi na kuwaambia watu kuwa wasimsikilize mtu fulani ambaye ukiangalia hajafikia daraja la kutahadharishwa lakini ukichunguza kwa makini utajua kuwa hiyo ni hila inayotumika na hawa ndugu zetu ili watu wasije kujua ukweli wa kile anachokizungumza mlinganiaji huyo na kubainikiwa na ubabaishaji wao !

Mwisho :

Kwa mfumo huu ambao hawa ndugu zetu wanaenda nao basi huko tunapoenda hakuna atakaye bakia katika suna bali kitakachotokea ni kugeukiana wao kwa wao ,na katika njia za kuliepuka hili ni kuwalea wanafunzi katika mfumo wa wema waliopita ambao ni mfumo Bora wenye sifa ya uadilifu na kuwatadharisha na uchupaji mipaka ambao madhara yake ni haya tunayoyaona leo hii Allah amuhifadhi sheikh Suleiman Arruhailiy ambaye aliwahi kuandika katika ukurasa wake wa twitter maneno yafuatayo :

الغلو في الدين، والأحكام،وتقدير الأمور، لا يجلب إلا شرا

Kuchupa mipaka katika dini,na (katika) hukumu ,na (katika) kukadiria mambo ,hakuna kinacholeta,isipokuwa ni shari,

فقد غلت الخوارج،

Na bila shaka walichupa mipaka Makhawariji,

ذلك فقتلت عصاباتهم الأولى عثمان – رضي الله عنه،

Na makundi yao ya kwanza (kuchomoza) yalimuua ‘Uthmaan-Allah amridhie-

في حرم المدينة،بعد تكفيره

Katika (mji) mtukufu wa Madinah,baada ya kumkufurisha,

ثم استحكم شرهم،

Kisha shari yao ikachukua nafasi,

بالخروج على علي ـ رضي الله عنه

Kwa kumuasi Alliy-Allah amridhie- (na kupambana naye)

ولازالت الأمة،بل الأرض كلها تعاني

Na ummah (wa kiislamu),
bali dunia yote inaendelea kupata shida (madhara),

من آثار غلوهم،

Kutokana na athari zao za kuchupa kwao mipaka,

وشرورهم وإجرامهم،

Na (kutokana) na shari zao na kufanya kwao maovu,

ولا حل، إلا بنشر الوسطية الشرعية .

Na wala hakuna utatuzi (ufumbuzi),
isipokuwa kusambaza ubora wa kisheria,

📚 كتبه الشيخ سليمان الرحيلي حفظه الله، “تويتر”

Ufafanuzi :

Makhawariji walichupa mipaka kwa kuwatia katika ukafiri waislamu na kuhalalisha damu zao na hivi ndivyo wanavyochupa mipaka baadhi ya ndugu zetu kwa kuwatia katika bidaa wale wasiostahiki, na bila shaka Uislamu unatahadharisha aina zote hizi za uchupaji mipaka .

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo sita 7, 1445H ≈ Sep /9, 2024M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz

         •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *