MAANA SAHIHI YA USHUJAA .

كتب الشيخ صالح العصيمي -حفظه الله تعالى- عبر حسابه على تويتر .

Ameandika sheikh Swaleh Al-Uswaim -Allah amuhifadhi- kupitia ukurasa wake wa twitter (maneno yafuatayo) :

من الخطأ في حقيقة الشَّجاعة توهُّم أنَّها جراءة اللسان أو ضخامة الأبدان،

Miongoni mwa makosa katika (kufahamu) ukweli wa ushujaa ni kudhania kuwa (ushujaa) ni urefu wa ulimi au ukubwa wa mwili

وإنَّما هي قوَّة القلب وثباته؛ بأن لا يزول عما يتحقَّقه، ولا يتحوَّل عما يتيقَّنه،

Na hakika si vingine (ushujaa) ni nguvu ya moyo na kuthibiti kwake (ktk mambo) kwa kutotoka katika lile ililolijua ukweli wa kulijua na wala usibadilike ukaliacha lile lililokuwa na yakini nalo,

فلا تخدعُه رقرقة العَبَرات، ولا تجتاله زخرفة العِبارات،

Na halitomhadaa bubujiko la machozi na wala hatozolewa na maneno yaliyopambwa,

ولا تكتسحه زلزلة الاضطرابات،

Na wala hatochukuliwa na tetemeko la wasiwasi

وقد تراه مع هذا حصِر اللسان ضعيف البدن.
Na unaweza ukamuona ni mwenye kuuzuia ulimi (wake) na mwenye mwili dhaifu .

الأحد ٢٦ ريع الأول ١٤٢٦ه‍

Maelezo ya mfasiri:

Sheikh -Allah amuhifadhi- anasema kuwa katika makosa ni watu kutofahamu maana sahihi ya ushujaa ni kule kudhania kwao kuwa ushujaa ni mtu kuwa na ulimi mrefu wa kuwasema watu wasio na makosa na kuzungumza bila kuchunga misingi ya kisheria, na kuchafua heshima zao na mimi naongeza kwa kusema hivi :

Tena wapo wafanyao hivi kwa nembo ya kuihami dini na kuingiza uwongo ndani yake, na pia watu wanadhania kuwa ushujaa ni mtu kuwa na mwili mkubwa ! kisha sheikh akaeleza kuwa maana sahihi ya ushujaa ni :

Ushupavu wa moyo na kuthibiti katika lile la haki aliloliju na kutobadilika kwa kuliacha lile alilolifahamu kwa yakini na kutohadaika na maneno ya watu wenye kuzungumza kwa masikitiko au kuyapamba maneno yao na kuingiza utata ili kuwatia watu wasiwasi katika ile haki waliyoshikamana nayo ,mwisho sheikh -Allah amuhifadhi-akamalizia maneno yake kwa kusema kuwa mtu huyu pamoja na ushujaa huu aliokuwa nao na ushupavu huu wa moyo wake unaweza ukamuona kuwa ni mtu mwenye kuuzuia ulimi wake, na umbile lake unaweza ukaliona ni dhaifu kimuonekano wa nje .

Bila shaka yule aliyeumiliki ulimi wake huyo ndiye shujaa wa kweli na Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie-amemsifu mtu huyu pale aliposema:

«طُوبَى لِمَنْ مَلَكَ لِسَانَهُ، وَوَسِعَهُ بَيْتُهُ، وَبَكَى عَلَى خَطِيئَتِهِ»

“ Heri nyingi kwa yule aliyeumiliki ulimi wake ,na ikamtosha nyumba yake na akalia juu ya makosa yake ”

رواه الطبراني في الكبير والصغير

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo saba 12 , 1445H ≈ Oct /15, 2024M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz

         •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *