قال تعالى :
Amesema Allah aliyetukuka:
﴿ وَلَا تَقْرَبُوا الزِّنَا ۖ إِنَّهُ كَانَ فَاحِشَةً وَسَاءَ سَبِيلًا﴾
Wala msikaribie zinaa. Hakika hiyo (zinaa) ni uchafu (mkubwa) na ni njia mbaya kabisa .
[ سورة الإسراء: ٣٢]
Amesema sheikh Abdul-Rahman Sa’ad- Allah amrahamu – :
والنهي عن قربانه أبلغ من النهي عن مجرد فعله لأن ذلك يشمل النهي عن جميع مقدماته ودواعيه فإن: ” من حام حول الحمى يوشك أن يقع فيه “
Na katazo la kuikaribia limeenda mbali zaidi kuliko katazo la kuifanya tu kwa sababu hilo (katazo la kuikaribia) linakusanya kukataza yote (ambayo ni) utangulizi wake na vichocheo vyake ,na bila shaka (inafahamika kuwa) :
Mwenye kuzunguka pembezoni mwa wigo basi anakaribia kuingia ndani yake
خصوصا هذا الأمر الذي في كثير من النفوس أقوى داع إليه.
Na haswa jambo hili ambalo katika nafsi nyingi kuna vichocheo vyenye nguvu vya kuliendea .
ووصف الله الزنى وقبحه بأنه كَانَ فَاحِشَةً أي: إثما يستفحش في الشرع والعقل والفطر
Na Allah ameuelezea uzinifu na ubaya wake kwamba ni uchafu, maana yake (ni jambo ambalo) linaonekana kuwa ni chafu kisheria na kiakili na kimaumbile
لتضمنه التجري على الحرمة في حق الله وحق المرأة وحق أهلها أو زوجها وإفساد الفراش واختلاط الأنساب وغير ذلك من المفاسد.
Kwa sababu ya (kule) kukusanya kwake kujitia ujasiri juu ya (kuvunja) utukufu katika haki ya Allah na haki ya mwanamke na haki ya familia yake au haki ya mumewe na kumchafulia kitanda na kuchanganyika nasabu na mengineyo katika ufisadi.
وقوله: وَسَاءَ سَبِيلًا أي: بئس السبيل سبيل من تجرأ على هذا الذنب العظيم.
Na kauli yake (Allah) :“ Na ni njia mbaya kabisa ” maana yake:
Njia mbaya kabisa ni njia ya yule aliyejitia ujasiri juu ya kufanya dhambi hii kubwa .
Maelezo ya mfasiri :
Bila shaka madhara ya uchafu huu wa uzinifu yapo wazi kwa kila mtu na ni madhara ambayo yanampata mwenyewe kwanza huyu mtoto wa nje ya ndoa na jamii kwa ujumla, na ndiyo maana mara nyingi ukiwaona watoto wa mtaani au wahuni basi watoto wa nje ya ndoa ndiyo wengi zaidi katika hao na utawakuta katika kila matukio mabaya wamejaa na hili ni kwa sababu mara nyingi huwa hawapati malezi bora kwa sababu ya kukosa kwao wazazi, hebu tusome maneno ya sheikh Aliyy Arramliy -Allah amuhifadhi- yanayobainisha ubaya wa dhambi hii na sababu zinazopelekea kukithiri dhambi hii :
أسباب كثرة أولاد الحرام في المجتمعات
نتيجة التبرج والسفور،
Sababu za kukithiri watoto wa haramu katika jamii ni matokeo ya (wanawake) kukaa uchi na kuacha hijabu
والاختلاط المحرم ، وكثرة خروج البنات من البيوت بغير رقيب ،
Na (kuwepo)michanganyiko ya haramu ,na wingi wa kutoka mabinti majumbani bila ya mwenye kuwachunga,
وتعطيل حدود الله في الأرض؛والوقوع في الزنا
Na kuacha kutekeleza adhabu (alizoziweka) Allah ulimwenguni (kwa waovu kama hawa), na kujiingiza katika uzinifu
فهذه طرقه التي سدها شرعنا، وأغلق بابها بإحكام.
Na hizi njia zake (zote ndizo) ambazo sheria yetu (ya kiislamu) imezizuia na ikafunga milango yake kwa umadhubuti .
والزنا يؤدي إلى كثرة قتل الأجنة بغير حق ، ووجود أولاد الحرام ،
Na uzinifu hupelekea (kutokea) wingi wa kuuliwa watoto bila ya haki, na kuwepo watoto wa haramu ,
وهؤلاء يحرمون من أقل حقوقهم الواجبة التي من أهمها فقد الأب بل والأم أحيانا ولا يخفاكم بعد ذلك ما يحصل من وراء ذلك من مفاسد .
Na hawa (watoto) hunyimwa miongoni mwa haki zao za chini kabisa za wajibu, na ya umuhimu zaidi katika hizo ni kukosa baba, bali na mama wakati mwingine na wala hayafichikani kwenu baada ya hayo yale yanayotokea nyuma ya hayo katika ufisadi.
فإما أن تهتم بهم الدولة ويكونون حملا ثقيلا عليها، أو يتركون يواجهون مجتمعا مليئا بالذئاب البشرية .
ima Serikali iwatilie umuhimu (kwa kuwatunza) ,na wanakuwa ni mzigo mzito kwa hiyo (serikali) , au (kama serikali) itawaacha (basi serikali) itakabiliana na jamii iliyojaa mbwa mwitu wa kibanadamu.
هذه المفاسد مِن وراء الزنا وأسبابه ؛
Huu uharibifu (uliopo) nyuma ya uzinifu, na sababu zake ni (hizi) :
يغض عنها الطرف الدعاة إلى حرية المرأة، وحرية الرأي، وحقيقة الأمر يبحثون عن حرية الشهوة الحيوانية .
(Na hapa) bila kujali walinganiaji wa uhuru wa mwanamke na uhuru wa mawazo, na uhakika wa jambo (watu hawa) wanatafuta uhuru wa matamanio ya kinyama
كما صرح أحد السياسيين في أستراليا ، قال: حجاب المرأة يمنعنا من التمتع بجمال المرأة .
Kama alivyoweka wazi (hilo) mmoja wa wanasiasa katika (nchi ya) Australia alisema (hivi):
Hijabu ya mwanamke inatuzuia na kujistarehesha na uzuri wa mwanamke .
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo tano 11, 1445H ≈ Aug /15, 2024M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•