Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net
🖋قال الشيخ عبدالرزاق بن عبد المحسن البدر -حفظه الله-:
Amesema sheikh Abdul-Rrazzaq ibn Abdil-Muhsin Al-badr- Allah amuhifadhi-:
“والسهر-ولا سيما في زماننا هذا- يعد من المصائب العظيمة، والبلايا الكبيرة، وله جنايات كثيرة على كثير من الناس،
Na kukesha na haswa katika zama zetu hizi huhesabiwa ni katika misiba mizito, na mabalaa makubwa (kukesha) kunawasababishia watu wengi (kuingia katika) makosa mengi ,
ومن أعظم الجنايات التي ترتبت عليه في زماننا هذا إضاعة صلاة الفجر،
na miongoni mwa makosa makubwa ambayo hutokana na huko (kukesha) katika zama zetu hizi ni kuipoteza swala ya Al-fajiri,
وهذه والله مصيبة جسيمة، فإذا نام الإنسان عن هذه الفريضة العظيمة فقد جنى على يومه جناية عظيمة.
na huu -naapa kwa Allah- ni msiba mkubwa ,basi mtu atakapolala na akaiacha faradhi hii tukufu bila shaka ameiingizia siku yake makosa makubwa .
📝قال ابن القيم رحمه الله:
Amesema ibn l-Qayyim- Allah amrahamu-:
((وأول النهار والشمس بمنزلة شبابه، وآخره بمنزلة شيخوخته، وهذا معلوم بالتجربة))،
Mwanzo wa mchana na (mwanzo wa) jua ni kama ujana wake ,na mwisho wake (ni kama) uzee wake na hili hujulikana kwa uzoefu .
ومن شب على شيء شاب عليه، فما يكون من الإنسان في أول اليوم ينسحب على بقيته؛ إن نشاطا فنشاط، وإن كسلا فكسل”.
na mwenye kukulia juu ya kitu (fulani) basi huzeekea juu (kitu) hicho, basi mtu anavyokuwa mwanzoni mwa siku yake huendelea kuwa (hivyohivyo) katika siku yake iliyobaki ikiwa (aliianza) kwa uchangamfu basi huwa mchangamfu (siku mzima) na kama (alianza) kwa uvivu basi huwa mvivu.
📓[شرح الشمائل المحمدية (ص٢٧٤).
Maelezo ya mtarjumu:
Kukesha kuna madhara makubwa sana madhara ya duniani na akhera ,na madhara makubwa zaidi ni kukosa swala ya Al-fajiri na mtu anapokosa kuswali swala ya Al-fajiri basi ajue kuwa siku hiyo ameianza vibaya ,kwa sababu mfano wa siku ni kama mwanadamu :
Mwanadamu pindi anapoleleka katika tabia fulani basi huzeeka hali ya kuwa ameshikamana na tabia hiyo , na hivyohivyo mtu anayepitwa na swala ya Al-fajiri basi atambue kuwa siku hiyo kwake ameianza vibaya .
Tanbih: Ni haramu kukesha kukiwa kutakupelekea kuikosa swala ya Al-fajiri hata kama mtu atakesha kwa kuswali ibada za sunnah au kutafuta elimu .
Na muislamu atambue kuwa kuamka mapema na kuswali swala ya Al-fajiri na kuanza kazi asubuhi mapema ni katika sababu ya kubarikiwa katika hiyo kazi ,kwa sababu Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie- aliwaombea dua wanao wahi mapema katika shughuli zao pale aliposema:
اللَّهمَّ بارِكْ لأمَّتي في بُكورِها.
Ewe Allah ubariki umati wangu katika kurauka kwake / kuwahi kwake asubuhi mapema
وَكانَ إذا بَعثَ سريَّةً أو جيشًا بَعثَهُم من أوَّلِ النَّهارِ
na alikuwa (Mtume-swala na salamu za Allah zimfikie-) anapotuma kikosi au jeshi hulituma mwanzoni mwa mchana /asubuhi
وَكانَ صخرٌ رجلًا تاجرًا، وَكانَ يَبعثُ تجارتَهُ من أوَّلِ النَّهارِ فأثرَى وَكَثُرَ مالُهُ
na alikuwa Swakhr -Allah amridhie- ni mtu mfanya biashara alikuwa akipeleka biashara yake mwanzoni mwa mchana /asubuhi basi akatajirika na zikakithiri mali zake .
صحيح أبي داود .
Ufafanuzi wa hadith:
Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie- alikuwa anapopeleka kikosi katika vita hukipeleka asubuhi mapema ili kupata baraka za kuwahi mapema , na mpokeaji wa hii hadithi Swakhr bin Wadaah’ Al-ghaamidiy-Allah amridhie- alikuwa ni mfanya biashara na yeye aliposikia maneno haya akawa anayafanyia kazi ili apate baraka ya dua hii ya Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie- akawa anapeleke biashara yake asubuhi mapema basi akatajiriki na mali zake zikakithiri.
Bila shaka mpaka hapa ndugu yangu muislamu utakuwa umejua umuhimu wa kurauka asubuhi mapema katika shughuli zako mbalimbali na kufanya hivyo ni katika sababu za kupata baraka ya dua ya Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie- , na vile vile utajua hasara ya kurudi tena kulala baada ya swala ya al-fajiri kwa sababu ni sababu ya kukosa baraka hizi na kuukosa muda huu uliobarikiwa, ila kukiwa na haja ya kurudi tena kulala baada ya Al-fajiri kama vile mgonjwa n.k .
Mtarjumu: Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo sita 27, 1443H ≈ November 2, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•