MAHD NI NANI ?

Kuna maneno yanayojiri katika baadhi ya mitandao ya kijamii katika kipindi hiki ambacho ndugu zetu wa Gazzah haswa na Wapalestina kwa ujumla wanapitia katika kipindi kizito na tunamuomba Allah awape faraja na awaangamize Mayahudi na washirika wao , maneno yenyewe ni haya kuna wanaosema kuwa hawa ndugu zetu watakuja kusaidiwa na Mahd na kuwashinda hao Mayahudi , je suala hili ni kweli ?

Ni kweli imethibiti kutoka kwa Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie- kuwa waislamu watapambana na Mayahudi na kuwashinda lakini hatujui ni kipindi gani ,lakini hili halitokei mpaka pale waislamu watapofuata dini yao kikamilifu, ama suala la kuja Mahd pia hili limethibiti lakini kipindi hicho ambacho Mahd -Amani iwe juu yake- atakapokuja baadae kidogo atashuka Isa mtoto wa Mariam-amani iwe juu yake – wote hao watashirikiana na waislamu wa kipindi hicho kuwapiga Mayahudi na Mayahudi watashindwa, lakini kusema kuwa Mahd atakuja sasa hivi bila shaka hilo sisi hatujui , kwa sababu kuja kwa Mahd na kushuka kwa Isa mtoto wa Mariamu hizi ni miongoni wa alama za kiama kubwa kubwa .

Na huyu Mahd ni nani ?

Lifuatalo ni jawabu kutoka kwa mwanachuoni mkubwa ibn Uthaimini-Allah amrahamu-:

أحاديث المهدي العلماء قسموها إلى أربعة أقسام :

Hadithi za (kuja) Mahdi wanavyuoni wamezigawanya vigawanyo vinne :

١- صحيحة.
٢- حسنة.
٣- ضعيفة.
٤- موضوعة.
1- Sahihi .

2-Hasan .

3-Dhaifu .

4- za uwongo .

✅ والراجح من أقوال أهل العلم: أنه سوف يأتي إذا دعت ضرورة الأرض إلى مجيئه.

Na kauli iliyokuwa na nguvu katika kauli za wanavyuoni kuwa (Mahd) atakuja pindi itapokuwa kuna dharura ya kuja kwake (hapa) ardhini.

كأن تُمْلأ ظلماً وجوراً؛

Kama vile (mfano) ardhi (ikiwa) imejazwa dhulma

ولكنه هذا المهدي الذي من عقيدة أهل السنة والجماعة ليس هو مهدي الرافضة الذي ينتظرونه.

Lakini huyo ni Mahd ambaye (kumuamini) ni katika itikadi ya Ahlu sunnah wal-jamah si yule Mahd wa Mashia ambaye wanamsubiri.

فإن مهدي الرافضة الذي ينتظرونه ليس إلا خيالاً في أذهانهم، ولا حقيقة له. فهم يعتقدون أن المهدي هذا في السرداب الذي في العراق،

Na bila shaka Mahd wa Mashia ambaye wanamsubiria hayupo isipokuwa ni mazingaombwe tu (yaliyopo) katika akili zao na wala si kweli, na wao (Mashia) wanaitikadi kuwa huyu Mahd yupo katika pango ambalo lipo Iraq,

وينتظرون خروجه كل يوم، وهذا لا أصل له، ولا حقيقة له، لا من الناحية التاريخية، ولا من الناحية العقلية.

na wao (Mashia) husubiria kutoka kwake kila siku , na hili (wanaloliamini) halina dalili na wala halina ukweli si katika upande wa kihistoria wala upande wa kiakili

🎙 المصدر: لقاء الباب المفتوح لابن عثيمين .

Ufafanuzi wa mfasiri:

Huyu ndiye Mahd ambaye atatokea mwishoni mwishoni mwa dunia kabla ya kushuka Isa mwana wa Mariam -Amani iwe juu yake- na kutokea kwake ni miongoni mwa alama za kiama kubwa kubwa ,Mahd ambaye atawaongoza waislamu na kuujaza ulimwengu uadilifu ,na kama alivyoeleza sheikh -Allah amrahamu- kuwa Ahlu sunnah tunaamini kuwa huyu Mahd atatokea na atakuwa ni katika kizazi cha Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie- kama alivyosema Mtume-swala na salamu za Allah zimfikie-:

” لا تقومُ السَّاعةُ حتى يَملِكُ رجُلٌ من أهلِ بَيْتي،

Hakitotokea Kiama mpaka amiliki (atawale) mtu katika watu wa nyumbani kwangu ,

أَجْلى أَقْنى، يَملَأُ الأرضَ عَدلًا، كما مُلِئَتْ قبْلَه ظُلمًا، يكونُ سَبعَ سنينَ “.

“ (sifa zake ni hizi) hana nywele mbele ya kichwa chake , paji lake la uso ni pana, mwenye pua ndefu iliyochongoka, ataujaza ulimwengu uadilifu kama (ulivyojazwa) kabla yake dhulma , na (utawala wake) utakuwa kwa muda wa miaka saba ”

أخرجه أحمد (١١١٣٠) واللفظ له، وأبو يعلى (١١٢٨).

Tanbih :

Shekhe -Allah amrahamu- ametoa tahadhari kuwa Mahd tunayemuamini sisi Ahlu ssunaah si yule wanayemuamini Mashia ambaye ni Mahd wa kubuni na wa uwongo na hayupo, na katika vituko vyao hao Mashia huwa wanamsubiria huyo Mahd huko Iraq katika pango wanadai kuwa atatoka huko na hili hulifanya kila siku !

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imetumwa kwa mara ya pili : Mfungo saba 10, 1445H ≈ Oct 25, 2023M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *