قال العلامة عبيد الله الجابري -رحمه الله تعالى-:
Amesema sheikh Ubaid-llah – A-jabir – Allah amrahamu :
فإن القرآن أنزل لمقاصد ثلاثة:
Hakika Quran imeteremshwa kwa makusudio matatu:
🔺- أحدها التعبد لله بتلاوته فكلما قرأ المسلم حرفًا كان له حسنة والحسنة بعشر أمثالها كما صح عن النبي صلى الله عليه وسلم من حديث عثمان رضي الله عنه،
(1) Kusudio la kwanza ni kumuabudu Allah kwa kuisoma, basi kila anaposoma muislamu herufi moja anakuwa na jema moja, na jema moja (hulipwa) kumi mfano wake kama ilivyothibiti kutoka kwa mtume- swala na salamu za Allah ziwe juu yake – kutoka kwa Uthman Allah amridhie,
روى هذا عن النبي صلى الله عليه وسلم.
Amelipokea hili kutoka kwa mtume swala na salam ziwe juu yake.
🔺- الثاني التدبر فإن التدبر هو آلة الفهم فبالتدبر يحصل الفهم وإذا حصل الفهم حصل العمل على الوجه الصحيح.
(2) (Kusudio) la pili ni kuizingatia, hakika bila shaka kuizingatia quran ndio nyenzo ya ufahamu, na kwa kuizingatia Quran hupatikana ufahamu wa hiyo (Quran), na ukipatikana ufahamu hupatikana kuifanyia kazi kwa sura iliyosahihi.
🔺- الثالث العمل به ولهذا كان الصحابة رضي الله عنهم لا يُجاوزون عشر آيات
حتى يتعلموا معناها والعمل بها.
(3) (Kusudio) la tatu ni kuifanyia kazi na kwa sababu hii walikuwa maswahaba – Allah awaridhie- hawavuki aya kumi mpaka wajifundishe maana yake na wazifanyie kazi.
المصدر : 📕مقتطف من شرح صحيح البخاري للشيخ عبيد الجابري – رحمه الله-
Maelezo ya mfasiri :
Tanbih :
Maana ya kauli yake Mtume _swala na salamu za Allah zimfikie :
مَنْ قرأَ حرفًا من كتابِ اللهِ فله به حسنةٌ ، والحسنةُ بعشرِ أمثالِها
Mwenye kusoma herufi katika kitabu cha Allah basi atapata kwa hiyo (herufi) jema moja, na jema moja (hulipwa) kumi mfano wake,
لا أقولُ آلم حرفٌ ، ولَكِن ألِفٌ حرفٌ، ولامٌ حرفٌ، وميمٌ حرفٌ
Na (mimi) sisemi (kuwa) alifu laam mmiim ni herufi lakini: alifu ni herufi, na lam ni herufi, na mimu ni herufi.
رواه الترمذي وغيره
Makusudio ya herufi kwa waarabu ni neno kwa maana kila unaposoma neno moja basi unalipwa thawabu kumi,mfano kauli yake Allah – aliyetukuka-:
إِنَّآ أَعۡطَيۡنَٰكَ ٱلۡكَوۡثَرَ
Hii aya ina herufi tatu kwa maana ina maneno matatu.
Kwa hiyo makusudio ya herufi hapa si herufi za hijaa kama vile :aliif, baau…
Tanbih: Faida nimeitoa katika darsa za sheikh Swaleh Al-uswaim – Allah amuhifadhi -.
Mfasiri : Ummu Aisha Asshafiyah-Allah amuhifadhi –
Maelezo na kupitiwa: Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo saba 20, 1445H ≈ Nov 4, 2023M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•