MALEZI YA WATOTO (NO.1)

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiya.net

MALEZI YA WATOTO (NO.1)

قواعد مهمة في تربية الأبنـاء.

☞ Misingi muhimu katika kuwalea watoto

يقول ابن القيم – رحمه الله –

Anasema Ibn l-Qayyim – Allah amrahamu –

١ – ومما يحتاج اليه الطفل غاية الاحتياج الاعتناء بأمر خلقه؛

1 – Na miongoni mwa yale anayoyahitajia mtoto upeo wa kuyahitajia ni kutilia umuhimu jambo la tabia yake;

فإنه ينشأ على ما عوده المربي في صغره،

Na bila shaka (mtoto) hukua juu ya vile alivyomzoesha mlezi utotoni mwake,

من غضب ولجاج وعجلة وخفة وطيش وجشع، فيصعب عليه في كبره تلافي ذلك،

Kama vile kukasirika na ubishi na haraka na upumbavu na kutokuwa makini na tamaa (uroho), basi inakuwa vigumu juu yake ukubwani kwake kuziacha (tabia) hizo,

ولهذا تجد أكثر الناس منحرفة أخلاقهم وذلك من قِبَل التربية التي نشأ عليها.

Kwa ajili hii utawakuta watu wengi zaidi waliopinda tabia zao hilo hutokana malezi ambayo waliokulia.

📚 تحفة المودود بأحكام المولود، (ص ١٥٨ – ١٥٩)

[ Tuhfatu l-mauduud biahkaamil – mauluud (ukurasa wa 158 – 159) ]

Maelezo kutoka kwa mfasiri – Allah amuhifadhi

Mzazi na mlezi chunga sana usije ukawa ni sababu ya kupotea mwanao na yule unayemlea kwa sababu mtoto huathirka na mazingira yanayomzunguka, hebu angalia ufafanuzi wa hilo katika swali hili aliloulizwa Sheikh Al-fauzan – Allah amuhifadhi –

معنى حديث:

Maana ya hadithi:

” كل مولود يولد على الفطرة فأبواه يهودانه أو يمجسانه أو ينصرانه “

“ Kila anayezaliwa huzaliwa katika maumbile basi wazazi wake wawili ndio wanao mfanya kuwa Myahudi au wanamfanya kuwa Mmajusi au wanamfanya kuwa Mnaswara ”

السؤال:

Swali: 🎤

هذا سائل يقول يا فضيلة الشيخ ما معنى حديث:

Huyu muulizaji anasema: ewe Sheikh mbora nini maana ya hadithi:

” كل مولود يولد على الفطرة فأبواه يهودانه أو يمجسانه أو ينصرنه “ ؟

“ Kila anayezaliwa huzaliwa katika maumbile basi wazazi wake wawili ndio wanao mfanya kuwa Myahudi au wanamfanya kuwa Mmajusi au wanamfanya kuwa Mnaswara? ”

الجواب:

Jawabu: 📚

معناه: أن كل مولود يولد وهو قابل لدين الإسلام لأن فطرته تتقبل هذا، قال جلَّ وعلا:

Maana yake: Kwamba kila mwenye kuzaliwa huzaliwa na hali ya kuwa ni mwenye kukubali dini ya kiislamu kwa sababu maumbile yake yanakubali hili, amesema (Allah) aliyetukuka na aliyekuwa juu:

{ فَأَقِمْ وَجْهَكَ لِلدِّينِ حَنِيفاً فِطْرَةَ اللَّهِ الَّتِي فَطَرَ النَّاسَ عَلَيْهَا }

{ Basi uelekeze uso wako kwenye dini hali ya kujitenga na dini za kishirikina ndio umbile la Allah ambalo amewaumbia watu }.

ولكن الفطرة قد تتغير بسبب التربية السيئة، فإذا كان أبوه يربيه على اليهودية صار يهودياً، إذا كان نصرانياً صار نصرانياً، وإن كان مجوسيا صار مجوسياً:

Lakini (hili umbile) huwenda likabadilika kwa sababu ya malezi mabaya, basi kama baba yake anamlea (mtoto) juu ya uyahudi atakuwa Myahudi na akiwa (baba yake) Mnaswara atakuwa Mnaswara, na akiwa Mmajusi atakuwa Mmajusi.

فأبواه يهودنه أو ينصرانه أو يمجسانه، الذي يحرف الفطرة السليمة هو التربية السيئة والتربية الخبيثة،

Basi wazazi wake wawili humfanya kuwa Myahudi au humfanya kuwa Mnaswara au humfanya kuwa Mmajusi, linalobadili maumbile yaliyosalimika ni malezi mabaya na malezi machafu,

فيجب على الوالدين أن يحرص على المحافظة على فطرة أولادهم الدينية، وأن يأمروهم بطاعة الله وينهوهم عن معصية الله، ويربوهم تربيةً إسلامية توافق فطرتهم، نعم.

Basi inawajibika juu ya wazazi wawili wapupie juu ya kuhifadhi (kutunza) maumbile ya watoto wao ya kidini, na wawaamrishe kumtii Allah na wawakataze kumuasi Allah, na wawalee malezi ya kiislamu yanayoafikiana na maumbile yao, ndio.

🔊 انتهى من ”موقع الشيخ الفوزان“

Yameisha maneno yake kutoka “mauqiu ya Sheikh Al-fauzaan”

Kiunganishi cha website ya Sheikh: https://www.alfawzan.af.org.sa

Ufafanuzi: yaani uislamu na tauhidi ndiyo maumbile ya mwanadamu, lau mtoto anapozaliwa akalelewa katika mazingira ya kumpwekesha Allah peke yake na kuepushwa na ushirikina na ukafiri basi huifuata njia hii kwa sababu ndiyo maumbile yake aliyoumbiwa na Allah, na vile vile tabia ya mtoto hupotezwa na mazingira anayoishi haswa wazazi wawili na walezi.

Itaendelea … 🖋

Muandaaji: fawaidusalafiya.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiya.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Iliandaliwa:January 2,2020 ikarudiwa tena Dhul-Qaadah 9, 1442H ≈ June 19, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *