https://t.me/fawaidussalafiyatz
Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiya.net
MALEZI YA WATOTO (NO. 02)
قواعد مهمة في تربية الأبنـاء.
☞ Misingi muhimu katika kuwalea watoto
يقول ابن القيم – رحمه الله –
Anasema Ibn l-Qayyim – Allah amrahamu –
٢- فيَجِبُ أن يُجنَّب الصبيُّ إذا عَقِل مجالسَ اللَّهو والباطل، والغناءِ وسماعِ الفُحْش، والبدع ومنطق السوء؛ فإنه إذا عَلِق بسمعِه عَسُر عليه مفارقتُه في الكِبَر، وعزَّ على وليِّه استنقاذُه منه، فتغييرُ العوائد من أصعب الأمور! يحتاج صاحبُه إلى استِجْداد طبيعةٍ ثانية، والخروج عن حكم الطبيعة عَسِرٌ جدًّا”؛
2 – Basi mtoto atakapo (fikia umri wa) kuwa na akili aepushwe vikao vya kipuuzi,
Na upotevu,
Na nyimbo (miziki),
Na kusikia machafu,
Na bida’a (uzushi)
Na matamko mabaya,
Na hakika hali ilivyo pindi (vitu hivi) vitakapong’ang’ania masikio yake huwa vigumu kuachana navyo kipindi cha ukubwani,
Na ni vigumu kwa mlezi wake kumuokoa katika (tabia) hiyo,
Na kuyabadilisha mazoea ni katika mambo magumu,
(Jambo hilo) anahitaji mhusika (mtoto) kuibadilisha tabia,
Na kutoka katika hukumu ya tabia (ya zamani) ni vigumu sana.
📚 تحفة المودود بأحكام المولود، (ص ١٥٨ – ١٥٩)
[ Tuhfatu l-mauduud biahkaamil – mauluud (ukurasa wa 158 – 159) ]
Nyongeza ya mfasiri – Allah amuhifadhi
Wazazi na walezi zingatieni sana malezi ya watoto, mtoto atakapolelewa malezi mabaya utotoni inakuwa ni vigumu kubadilika hapo baadaye, kwa sababu kile kinachopandikizwa katika moyo wa mtoto katika kipindi cha utotoni mwake hukita (hung’ang’ania) sawa sawa,
Kuna methali ya kiswahili inayosema:
“ Samaki mkunje angali mbichi ”
Na mshairi wa kiarabu anasema:
وينشأ ناشيئ الفتيان منا،
Na hukua mwenye kukua katika sisi vijana,
على ما كان عوده أبوه.
Juu ya vile alivyomzoesha baba yake.
Itaendelea … 🖋
Muandaaji: fawaidusalafiya.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiya.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Iliandaliwa: January 3,2020 ikarudiwa tena Dhul-Qaadah 10, 1442H ≈ June20, 2021M.
#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•