Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiya.net
MALEZI YA WATOTO (NO. 05)
قواعد مهمة في تربية الأبنـاء.
☞ Misingi muhimu katika kuwalea watoto
يقول ابن القيم – رحمه الله –
Anasema Ibn l-Qayyim – Allah amrahamu –
ويُجَنِّبُهُ الْكَسَلَ والبطالة والدعة والراحة بل يأخذه بأضدادها ولا يريحه إلا بما يجم نفسه وبدنه للشغل فإن الكسل والبطالة عواقب سوء ومغبة ندم وللجد والتعب عواقب حميدة إما في الدنيا وإما في العقبى وإما فيهما فأروح الناس أتعب الناس وأتعب الناس أروح الناس فالسيادة في الدنيا والسعادة في العقبى لا يوصل إليها إلا على جسر من التعب قال يحيى بن أبي كثير لا ينال العلم براحة الجسم
ويعوده الانتباه آخر الليل فإنه وقت قسم الغنائم وتفريق الجوائز فمستقل ومستكثر ومحروم فمتى اعتاد ذلك صغيرا سهل عليه كبيرا
5 – Na (mzazi/mlezi) amuepushe (mtoto) na uvivu na kukaa bila kazi na starehe na raha,
Bali amchukue (kwa kumfanyisha) kinyume cha hayo na wala asimstareheshe (mtoto),
ila kwa (kiwango) ambacho kinaipumzisha nafsi yake na mwili wake kwa ajili ya kazi,
Na bila shaka uvivu na kutojishughulisha vina mwisho mbaya na mwisho (wenye) majuto,
Na kujitahidi na tabu vina mwisho mzuri,
ima katika dunia ima akhera ima kote (duniani na akhera),
Basi watu wenye kustarehe zaidi ni wale wenye kupata tabu zaidi,
Na watu wenye kupata tabu zaidi ni watu wenye starehe zaidi,
Basi utulivu (starehe) duniani na utulivu akhera havifikiwi ila kwa (kuvuka) daraja la tabu.
Amesema Yahyaa bin Abii Kathiir:
{ Elimu haipatikani kwa raha ya kiwiliwili }.
Na (mzazi/mlezi) amzoeshe (mtoto) kuamka mwishoni mwa usiku (kwa kuswali)
Na hakika (muda) huo ni wakati wa kugawanywa ngawira na (muda) wa kugawanywa zawadi,
Basi (kuna) mwenye kupata (ngawira) kwa uchache na mwenye kupata kwa wingi , na kuna mwenye kunyimwa (ngawira).
Basi muda ambao (mtoto) atakapozoea hilo hali ya kuwa ni mtoto litawepesika juu yake hali ya kuwa ni mkubwa.
📚 تحفة المودود بأحكام المولود، (ص ١٥٨ – ١٥٩)
[ Tuhfatu l-mauduud biahkaamil – mauluud (ukurasa wa 158 – 159) ]
Maelezo kutoka kwa mfasiri – Allah amuhifadhi
Usimlee mtoto katika maisha ya raha na kubweteka na uvivu bali mlee katika maisha ya kuchapa kazi na kujitahidi katika kazi za dunia na akhera, kwani huwezi kupata utukufu duniani au akhera ila kwa kujipinda,
Hata ukiangalia historia ya wanachuoni wakubwa duniani waliopita na wa zama hizi utaona kwamba wamejipinda mno mpaka wakaipata hiyo elimu na kuna wale ambao walikuwa hawalali isipokuwa kiasi cha kupumzisha miili yao kama vile imamu Annawawiy – Allah amrahamu – na wengineo,
Na pia mzazi anatakiwa amzoeshe mwanae kuamka mwishoni mwa usiku muda ambao Allah huteremka katika uwingu wa dunia na kuwajibu watu maombi mbalimbali na kuwapa watu msamaha huu ni muda muhimu mno muda ambao kuna watu hupewa mengi kutoka kwa Allah ,na kuna wanaopewa machache na kuna wale wasiopewa chochote kwa sababu ya uvivu wao wa kuamka ,kwa hiyo mzazi amzoeshe mwanaye pindi atakapofikia umri wa kupambanua na zaidi kidogo,
Lakini atumie njia nzuri katika hili kwa sababu hili ni jambo la sunnah asimchape, na mfahamishe kwamba tabu anazozipata ni sababu ya kustarehe duniani na akhera kama anavyosema mshairi:
بقدر الكد تكتسب المعالي،
Kwa kadri ya juhudi hupatikana mambo ya juu (matukufu),
ومن طلب العلا سهر الليالي،
Na mwenye kutaka mambo ya juu hukesha usiku,
ومن رام العلا من غير كد،
Na mwenye kukusudia mambo matukufu (ya juu) bila ya juhudi,
أضاع العمر في طلب المحال،
Atapoteza umri katika kutafuta kisichowezekana ,
تروم العز ثم تنام ليلا!؟
Unakusudia utukufu kisha unalala usiku!?
يغوص البحر من طلب اللآلي.
Huzama baharini mwenye kutafuta lulu.
Itaendelea … 🖋Allah akitaka .
Muandaaji: fawaidusalafiya.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiya.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Dhul-Qaadah 12, 1442H ≈ June, 22, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•