https://t.me/fawaidussalafiyatz
Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiya.net
MALEZI YA WATOTO (NO. 06)
قواعد مهمة في تربية الأبنـاء.
☞ Misingi muhimu katika kuwalea watoto
يقول ابن القيم – رحمه الله –
Anasema Ibn l-Qayyim – Allah amrahamu –
ويجنبه فضول الطعام والكلام والمنام ومخالطة الأنام فإن الخسارة
في هذه الفضلات وهي تفوت على العبد خير دنياه وآخرته
6 – Na (mzazi/mlezi) amuepushe (mtoto) na (tabia ya) kuzidisha kula , na mazungumzo, na kulala, na kuchanganyika na watu,
Basi bila shaka hasara (ipo) katika hizi ziada,
na hizo (ziada) zinamkosesha mja heri za dunia yake na akhera yake,
ويجنبه مضار الشهوات المتعلقة بالبطن والفرج غاية التجنب فإن تمكينه من أسبابها والفسح له فيها يفسده فسادا يعز عليه بعده صلاحه
Na (mzazi/mlezi) amuepushe (mtoto) na madhara ya matamanio yanayoambatana na tumbo na utupu ukomo wa kumuepusha,
Na bila shaka kumuwezesha (mtoto) kwa (kuyafanya hayo) na akampa idhini ya (kuyafanya) hayo atamuharibu uharibifu (mkubwa) itakuwa ni vigumu baada ya hapo kutengemaa kwake,
وكم ممن أشقى ولده وفلذة كبده في الدنيا والآخرة بإهماله وترك تأديبه وإعانته له على شهواته ويزعم أنه يكرمه وقد أهانه وأنه يرحمه وقد ظلمه وحرمه ففاته انتفاعه بولده وفوت عليه حظه في الدنيا والآخرة وإذا اعتبرت الفساد في الأولاد رأيت عامته من قبل الآباء
Ni wangapi ambao wamewafanya watoto wao kuwa waovu,
na (hao watoto ni) kipande cha maini yao duniani na akhera,
(wamewafanya kuwa waovu) kwa kuwapuuza na kuacha kuwaadabisha,
na kuwasaidia kwao hao (watoto) juu ya matamanio yao (machafu),
na (wanafanya hivyo) na hali ya kuwa wanadai kuwa wanawakirimu na bila shaka wamewadhalilisha hao (watoto)
na (wanadhani) kuwa wanawafanyia huruma na bila shaka (kwa hakika) wamewadhulumu na kuwanyima (haki zao),
wakapitwa na kunufaika nao na wakawakosesha (watoto wao) fungu lao duniani na akhera.
Na pindi utakapozingatia uharibifu katika watoto utaona wengi wao hutokana na mababa (wazazi).
📚 تحفة المودود بأحكام المولود، (ص ١٥٨ – ١٥٩)
[ Tuhfatu l-mauduud biahkaamil – mauluud (ukurasa wa 158 – 159) ]
Maelezo kutoka kwa mfasiri – Allah amuhifadhi
Mzazi asimlee mwanae kwa kukithirisha haya aliyoyataja Sheikh ambayo ni:
1 – Kula sana yaani kukithirisha kula.
2 – Kukithirisha kuzungumza.
3 – Kukithirisha kulala.
4 – Kukithirisha kuchanganyika na watu.
Kuzidisha katika hivi vitu kuna hasara kubwa duniani na akhera.
5- Muepushe na mkinge na sababu za kujifundisha machafu ya utupu /uzinifu ,liwati ,maovu ambayo ni sababu ya kuadhibiwa duniani kabla ya akhera haswa liwati .
Mfano kukithirisha kula yaani ulafi! ulafi unamadhara mengi kama vile uvivu na huwenda ikawa ni sababu ya baadhi ya maradhi au kupitwa na mambo ya msingi kwa sababu ya kutilia umuhimu kula.
Kukithirisha kuongea ni balaa! kwa sababu ndio sababu ya kuingia katika makosa ya ulimi kama vile kusengenya, kuongopa, umbea, au akaingia katika kupiga porojo.
Kulala kupita kiasi athari yake ni mbaya sana kwa sababu huwezi ukapata baadhi ya mazuri mpaka uache kulala kupita kiasi, mfano vipi ataweza kuwa mjuzi wa dini yake yule ambaye hulala kama pono!?
Kuchanganyika na watu sana ni njia au sababu ya kuiga tabia zao haswa mtoto, mzazi/mlezi muepushe mtoto asichanganyike na watu sana, je wale wazazi wanao wabwaga watoto wao katika vituo vya kulelea watoto kuanzia asubuhi mpaka jioni hivi hali ya hawa watoto itakuwa vipi baadaye !?
Tanbih: Usimlee mtoto kwa kumpa kila anachokitaka ukadhania kwamba unamkirimu kumbe una muangamiza! na kumbuka kuwa mwanao usipomlea vizuri umemuangamiza duniani na akhera na unajinyima fursa ya kunufaika naye duniani na akhera au unaweza ukanufaika naye duniani pekee, na tambua kwamba watoto wengi wameharibika kwa sababu ya wazazi.
Itaendelea … 🖋Allah akitaka .
Muandaaji: fawaidusalafiya.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiya.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Dhul-Qaadah 13, 1442H ≈ June 23, 2021M.
#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•