MAMBO MAWILI YANAYOMUAJIBISHIA MTU KUINGIA PEPONI AU MOTONI .

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net

🎋➠
MAMBO MAWILI YANAYOMUWAJIBISHIA MTU KUINGIA PEPONI AU MOTO ?

📌 عَنْ جَابِرٍ رضـﮯ الله عنه قَالَ: أَتَى النَّبِـﮯَّ صلى الله عليــہ وسلم رَجُلٌ، فَقَالَ يَا رَسُولَ اللَّهِ:

Kutoka kwa Jabir- Allah amridhie-: amesema:

Kuna mtu alikuja kwa Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie- na akasema: Ewe Mjumbe wa Allah :

❐ مَا الْمُوجِبَتَانِ؟

Ni mawili yapi yenye kuwajibisha ?

فقال : ( مَنْ مَاتَ لَا يُشـــْرِكُ بِاللَّهِ شَيْئًا دَخَلَ الْجَنَّـــةَ، وَمَنْ مَاتَ يُشـــْرِكُ بِاللَّهِ شَيْئًا دَخَلَ النَّارَ ) .

Basi akajibu (Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie-):

{ Ambaye amefariki na hali hamshirikishi Allah na chochote ataingia peponi, na ambaye amefariki na hali anamshirikisha Allah na chochote ataingia motoni}

📓📔 رواه مسلم ( ٩٣ )

📌 قال الإمام النـــووي الشافعي رحمـہ الله:
Amesema imamu Annawawiy Asshafiy- Allah amrahamu-:

❐ أَمَّا قَوْله ( مَا الْمُوجِبَتَانِ ؟ ) فَمَعْنَاهُ الْخَصْلَـــة الْمُوجِبَـــة لِلْجَنَّــةِ، وَالْخَصْلَة الْمُوجِبَـة لِلنَّارِ.

Ama kauli yake (yule mtu): (Ni mawili yapi yenye kuwajibisha ?) maana yake jambo linalowajibisha pepo ,na jambo linalowajibisha moto .

▣ المصــدر :

📓📔شرح صحيح مسلم 【 ٢/٩٦ 】

Maelezo ya mtarjumu:

Maana ya hadithi ni kuwa:

Yeyote atakayefariki na hali ameepukana na ushirikina mkubwa na ukafiri basi mtu huyo makazi yake ni peponi milele hata kama ataadhibiwa motoni kwa muda lakini atatolewa na ataingizwa peponi ,kwa maana Allah amemuajibishia pepo kwa ukarimu wake Allah na ihsani yake .

Na yeyote atakayefariki hali anamshirikisha Allah ushirikina mkubwa kama kuabudia masanamu ,makaburi kwa kuwaomba maiti,au mizimu na aina nyingine za ushirikina au atakayekufa hali anamkufuru Allah basi mtu huyo makazi yake ni motoni milele na huu ni uadilifu wa Allah.

Mtarjumu: Ismail Seiph Mbonde .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Swafar/Mfungo tano 10, 1443H ≈ September 17, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *