MANENO YANAYOSTAHIKI KUANDIKWA KWA WINO WA DHAHABU.

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net

قال الشيخ_النجمي – حفظه الله تعالى :

Amesema sheikh Annajmiy- Allah aliyetukuka amrahamu-:

《وليست السلفية عندنا تقليد رجل من الرجال المعاصرين في كل ما يقوله ويفتي به فمثل هذا النوع من التقليد نعتبره لوناً من ألوان الحزبية الضيّقة

Usalafi kwetu si kumuiga mtu (mmoja) katika watu wa zama hizi katika kila anachosema na anachotoa fatwa, basi mfano wa aina hii ya uigaji tunauzingatia ni aina katika aina za uhizbi unaobana,

وشكلا من أشكال التعصب المذهبي المذموم والعالم مهما علا شأنه وعم فضله وعلمه لابد أن نأخذ من قوله ونرد》.

na ni sura katika sura za ubaguzi wa kimadhehebu (ambao) ni mbaya, na mwanachuoni vyovyote litakavyokuwa juu jambo (daraja) lake, na ukaenea ubora wake na elimu yake hakuna budi tuchukue kutoka kwake (ya haki) na tuyakatae (yasiyokuwa ya haki)

📚المورد العذب الزلال ٢٨٩

Maelezo ya mtarjumu:

Sheikh -Allah amrahamu- anaeleza kuwa :Njia ya wema waliopita si kumfuata shekhe fulani katika kila analolisema kana kwamba hakosei,bali kufanya hivi ni katika aina ya kutengeneza kikundi (uhizbi) ,ni sawa sawa na ule ubaguzi wa kimadhehebu ya fiqihi mtu akawa anaitikadi kuwa madhehebu yaliyosawa ni ya imamu fulani pekee ! na sheikh akaeleza kuwa kila mwanachuoni hupatia na kukosea na sisi tunachukua alilopatia na kuacha makosa yake ,na haya aliyoyazungumza sheikh anawakusudia wanachuoni wakubwa , na ikiwa haifai kuwa na ubaguzi kwa wanachuoni wakubwa basi bila shaka kuwa na ubaguzi kwa walinganiaji mbalimbali au walimu au wanafunzi wanaofundisha elimu ya kisheria bila shaka hilo ni baya zaidi kwa sababu ikiwa ubaguzi umekatazwa kwa wanachuoni wakubwa ambao ni marejeo ya ummah katika kadhia kubwa kubwa, je kwa asiyekuwa mwanachuoni, ambaye anazingatiwa ni mwanafunzi mbele ya wanachuoni, ambaye hata hawazingatiwi kuwa ni marejeo ?!.

Bila shaka tabia hii haifai na pia inatengeneza kikundi kinachobana na kuifinya haki na kuifanya haki kuwa ipo kwa sheikh fulani pekee au mlinganiaji fulani,au mwalimu fulani na matokeo yake ni watu kuchukiana na kutengana na kuna hatari kubwa ya kumegeka vikundi vikundi na kukatokea uadui mkubwa baina yetu , na Allah amesema katika kukemea hili:

مُنِيبِينَ إِلَيْهِ وَاتَّقُوهُ وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَلَا تَكُونُوا مِنَ الْمُشْرِكِينَ

Nyeyekeeni kwake (Allah) na mcheni Allah, na simamisheni swala, na wala msiwe katika washirikina .

مِنَ الَّذِينَ فَرَّقُوا دِينَهُمْ وَكَانُوا شِيَعًا ۖ كُلُّ حِزْبٍ بِمَا لَدَيْهِمْ فَرِحُونَ

Katika wale walioitenga dini yao na wakawa makundi makundi; kila kikundi kinafurahia kile kilicho nacho .

سورة الروم (٣١-٣٢) .

Kwa kifupi usalafi /kufuata mfumo wa wema waliopita kwa maana kuufuata ule uislamu halisi alioufundisha Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie- ,huu usalafi haufungwi na mtu wala sehemu bali usalafi ni mfumo wa wema waliopita kama anavyosema sheikh ibn Uthaimin- Allah amrahamu-:

فأهل السنة والجماعة هم السلف معتقدًا ،

Basi Ahlu sunnah wal-jamaa hao ndio Masalafi kiitikadi,

حتى المتأخر إلى يوم القيامة إذا كان على طريقة النبي – صلى الله عليه وسلم- وأصحابه ؛فإنه سلفيٌّ .

hata yule aliyekuja baadae mpaka siku ya kiama, pindi atakapokuwa katika mfumo wa Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie- na maswahaba wake basi (muislamu) huyo ni salafi .

شرح العقيدة الواسطية ص: ٣١

Mtarjumu: Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Swafar (Mfungo tano) 28, 1443H ≈ October 5, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *