Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net
MAPENZI YA KWELI YA WANANDOA WAWILI WALIOPENDANA KWA AJILI YA ALLAH HUDUMU HATA BAADA YA KIFO!
SOMA KISA HIKI CHENYE MAZINGATIO .
ماتت زوجة العلّامة المؤرخ المقريزي وهي شابة،
Alifariki mke wa mwanachuoni mkubwa, mwanahistoria Al-maqriiziy na hali huyo (mke) ni kijana,
فترجم لها، وقال
Basi (Al-maqriziy) aliandika historia ya huyo (mkewe), akasema:
وكنت أكثر الاستغفار لها، :
Na (alipofariki) nilikuwa nikikithirisha kumtakia msamaha,
فأُرِيتها في المنام فقلت لها:
يا أمّ محمد الذي أرسله إليك يصل أي الاستغفار ،
basi nikaoneshwa katika ndoto nikimwambia:
Ewe mama Muhammad je, kile ninachokutumia kinakufikia -anakusudia msamaha anaomuombea-,
قالت:
نعم، في كل يوم تصل هديتك
إليَّ،
akajibu:
Ndio, kila siku inanifikia zawadi yako kwangu,
ثم بكت! وقالت: قد علمتَ أنِّي عاجزة عن مُكافأتك
Kisha akalia!( mke )na akasema:
Bila shaka unajua kwamba mimi sina uwezo wa kukulipa,
فقلت لها: لا عليك ..عمّا قليل نلتقي
Basi nikamwambia:
Usijali .. baada ya muda mchache tutakutana.
📚 درر العقود الفريدة.
[ Duraru l-‘uquud -l-fariidah ]
Faida Kutoka kwa mfasiri – Allah amuhifadhi
Aliyelala huviona vitu vya aina tatu katika ndoto:
1- Ndoto inayotoka kwa Allah kama vile huwenda mtu akaliona jambo analolipenda katika ndoto na huwenda ikawa makusudio yake ni kupewa bishara njema au kutahadharishwa na shari au kupewa msaada au kupewa muongozo fulani, na pindi mtu atakapoona ndoto kama hii inasuniwa amshukuru Allah na awasimulie vipenzi vyake na wenye sifa ya ufahamu mzuri , na asiwasimulie wale wasiompenda kama wenye husuda ,na chuki .
2 – Ndoto inayotokana na shetani! hutokea mtu akaona usingizini mambo yanayochukiza na yanayokera, kinachotakiwa ni mtu ajikinge kwa Allah kutokana na huyo shetani na ateme vijimate kushotoni kwake mara tatu ila kama upande huo kuna mtu amelala kama mkewe basi asiteme atosheka na kujikinga kwa na Allah, na asimsimulie mtu yeyote na haitomdhuru , na vile vile ni sunnah ageukie upande mwengine yaani kama alikuwa amelalia upande wa kulia basi ageukie upande wa kushoto na pia ni sunnah atawadhe na aswali rakaa mbili.
3 – Ndoto inayotokana na mawazo yaliyopo katika nafsi ya mtu, mfano mtu aliyekuwa anawaza safari fulani muda wote kisha baada ya kulala akaona ndotoni kuwa anasafiri hizi zinaitwa ndoto zilizoparaganyika yaani si safi bali ni mawazo ya mchana tu.
Tanbihi muhimu sana:
Usiishughulishe akili yako na ndoto ukawa kila unaloliona katika ndoto unataka utafsiriwe pia si kila mtu anajua kutafsiri ndoto, na pia ndoto haiwezi ikawa dalili ya hukumu ya kisheria isipokuwa ndoto za mitume tu ambazo ni ufunuo kutoka kwa Allah.
Pia kuna kitabu ambacho kimeenea madukani kinaitwa:
تعبير الرؤيا.
Kutafsiri ndoto
Kitabu hiki kinanasibishwa na Ibn Siiriin hali ya kuwa si kweli, kwa maana Ibn Siiriin – Allah amrahamu – hakutunga kitabu hiki.
Muandishi Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Toleo la kwanza: August 19,2019M, toleo la pili: Mfungo sita 8, 1443H ≈ October 14, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•