Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiya.net
MAPENZI YAKO YA ALLAH YANADHIHIRI KATIKA MAENEO MANNE :
🌷قال الإمام ابن القيم رحمه الله:-
🍃 أربعة مواطن تُظهر مقدار تعلق ومحبة العبد لربه
Amesema imamu ibn l-Qayyim -Allah amrahamu-: –
Maeneo manne hudhihirisha kiwango cha mahusiano na mapenzi ya mja kwa Mola wake mlezi :
🌷أحدها :
🍃عند أخذ مضجعه وتفرغ حواسه وجوارحه الشواغل واجتماع قلبه على ما يحبه.
🍃 فإنه لا ينام إلا على ذكر من يحبه وشغل قلبه به ..
(Sehemu) yake ya kwanza :
Pindi anapolala na pindi viungo vyake vya fahamu na viungo vyake (vingine) vinapomaliza shughuli na moyo wake unapojikusanya pamoja na vile anavyovipenda .
basi bila shaka yeye (mwanadamu) halali isipokuwa kwa kumtaja yule anayempenda na kuushughulisha moyo wake na huyo (anayempenda) ..
🌷 الموطن الثاني :
🍃عند انتباهه من النوم ، فأول شيء يسبق إلى قلبه ذكر محبوبه ،
🍃 فإنه إذا استيقظ وردت إليه روحه رد معها إليه ذكر محبوبه الذى كان قد غاب عنه فى النوم ..
Sehemu ya pili : Pindi anapozinduka kutoka usingizini ,basi kitu cha kwanza kinachotangulia katika moyo wake ni kumtaja (kumkumbuka) kipenzi chake ,kwa sababu yeye (mwanadamu) pindi anapoamka na akarudishiwa roho yake ,hurudishiwa pamoja na hiyo (roho) kumbukumbu ya kumkumbuka kipenzi chake ambaye alikuwa ametoweka kwake katika usingizi .
🌷 الموطن الثالث:
🍃عند دخوله فى الصلاة ، فإنها محك الأحوال وميزان الإيمان ،
🍃 بها يوزن إيمان الرجل و يتحقق حاله ومقامه ومقدار قربه من الله ونصيبه منه ..
Sehemu ya tatu : Pindi anapoingia katika swala ,bila shaka hiyo (swala) ni sehemu kujaribiwa hali ya (watu) na ndiyo mizani ya imani ,kwa hiyo (swala) hupimwa imani ya mtu na huthibiti hali yake na nafasi yake na kiwango cha ukaribu wake na Allah ,na fungo lake kutoka kwa (Allah) ..
🌷 الموطن الرابع :
🍃عند الشدائد والأهوال ،
🍃فإن القلب فى هذا الموطن لا يذكر إلا أحب الأشياء إليه ، ولا يهرب إلا إلى محبوبه الأعظم عنده ..
Sehemu ya nne : Wakati wa shida na vitisho (misukosuko) ,bila shaka moyo katika sehemu hii haukitaji isipokuwa kitu kinachopendeza zaidi kwake na haukimbilii isipokuwa kwa yule anayempenda zaidi ..
المصدر :
🌷 طريق الهجرتين : (٣٠٦/١).
Maelezo:
Haya ni maeneo manne ambayo mwanadamu humtaja na kumkumbuka yule anayempenda na kama akiwa mwanadamu anamtaja na kumkumbuka Allah basi hiyo ni dalili ya mapenzi yake kwa Allah, na hayo maeneo ni :
1- Pindi anapolala, nao ni muda ambao viungo vyake vyote huwa vimemaliza kazi zake ,na ni muda ambao moyo wa mwanadamu huwapamoja na vile anavyovipenda kwa kuvitaja na kuvikumbuka ,na muda huu moyo ukimtaja Allah na kumkumbuka hii ni dalili ya moyo huo kuwa unampenda Allah .
2- Pindi anapoamka usingizini .
3-Anapokuwa katika swala na swala ndiyo majaribio ya kujulikana mapenzi ya mwanadamu kwa Allah .
4- Katika shida na misukosuko ,muda ambao mwanadamu hukimbilia kwa yule anayempenda zaidi .
Muandaaji: fawaidusalafiya.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiya.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Shawwal 21, 1442H ≈ Jun 2, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•