Masiku kumi ya mwanzo ya mwezi wa Mfungo tatu.

مسألة حسنة:
Masuala mazuri:

اختلف في أيهما أفضل، هل ليالي العشر الأواخر من رمضان أم ليالي العشر الأُول من ذي الحجة؟

Kumetokea tofauti katika (masuala haya): Ni yepi kati ya mawili hayo yana ubora zaidi, je ni masiku kumi ya mwisho ya mwezi ya Ramadhani au masiku kumi ya mwanzo ya mwezi wa Mfungo tatu ?

🟢فقيل بالأول؛ لأنَّ فيها ليلة القدر.
🟢وقيل بالثاني؛ لأن الله أقسم بها، فقال:

﴿ وَلَيَالٍ عَشْرٍ ﴾

Na kukasemwa (kauli) ya kwanza (kuwa masiku kumi ya mwisho ya mwezi wa Ramadhani yana ubora zaidi) : kwa sababu ndani yake kuna usiku wa cheo ,na kukasemwa (kauli) ya pili (kuwa masiku kumi ya mwanzo ya mwezi wa Mfungo tatu yana ubora zaidi) kwa sababu Allah ameapa kwa (masiku) hayo akasema:

{Naapa kwa masiku kumi}

قال شيخ الإسلام زكريا في منحة الباري (٣/٤٣):
Amesema sheikh l-slam Zakariyyah katika kitabu (chake) Minhatul-Baariy (3/43) :

(والتحقيق ما قيل: أنَّ العشر أفضل من مجموع عشر رمضان،

Na (kauli) iliyochunguzwa na ikapewa nguvu ni ile iliyosemwa kuwa: Masiku kumi ya mwanzo ya mwezi wa Mfungo tatu yana ubora zaidi ya mjumuiko wa Masiku kumi ya mwisho ya mwezi wa Ramadhani.

وإن كان في عشره ليلةٌ لا يفضل عليها غيرها؛ لقوله تعالى

na pamoja na kwamba katika masiku yake kumi kuna usiku (ambao) hakuna siku inayouzidi ubora usiku huo kwa kauli yake (Allah) aliyetukuka- :

﴿لَيْلَةُ ٱلْقَدْرِ خَيْرٌ مِّنْ أَلْفِ شَهْرٍۢ﴾

{Usiku wa cheo ni mbora kuliko miezi elfu moja}

                 •••●◆❁🌸🌼🌸❁◆●•••

Maelezo ya mfasiri:

Wanawachuoni wametofautiana katika hili:

Ni yepi masiku yenye ubora zaidi kati ya masiku kumi ya mwisho ya Ramadhani na masiku kumi ya mwanzo ya Mfungo tatu?

Kauli ya kwanza : Kuna wale waliosema kuwa masiku kumi ya mwisho ya Ramadhani yana ubora zaidi kwa sababu ndani yake kuna usiku wa cheo ambao una ubora kuliko miezi elfu ambayo sawa na miaka 83 na miezi 4, kwa maana ibada zinayofanywa usiku huo mmoja zinalingana na ibada zilizofanywa katika miezi elfu ambayo haina usiku wa cheo .

Kauli ya pili: Kuna wale waliozichunguza kauli zilizosemwa katika hili kisha wakachanganua wakasema hivi:

Masiku kumi ya mwanzo ya Mfungo tatu yana ubora zaidi ya mjumuiko wa masiku kumi ya mwisho ya Ramadhani maana yake ni kwamba :Ukiangalia masiku kumi ya mwanzo ya mwezi wa Mfungo tatu na ukiyaangalia masiku kumi ya mwisho ya Ramadhani kwa ujumla wake utaona kuwa masiku kumi ya mwanzo ya mwezi wa Mfungo tatu yana ubora zaidi ya yale masiku kumi ya mwisho ya Ramadhani, isipokuwa ndani ya hayo masiku kumi ya mwisho ya Ramadhani kuna usiku wa cheo ambao ubora wake ni wa kipekee na hakuna siku inayozidi ubora wa siku hiyo.

Nyongeza:

Kama walivyoeleza wanawachuoni kuwa katika yale yanayojulisha ubora wa masiku kumi ya mwanzo ya mwezi wa Mfungo tatu kwamba Allah ameapa kwa masiku haya katika Suratul-fajir na pia yamekuja maneno ya Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie -yanayojulisha kuwa ibada inayofanywa katika masiku haya inapendeza zaidi mbele ya Allah na pia akaeleza katika hadithi nyingine akasema kuwa:

أفضلُ أيامِ الدنيا أيامُ العشْرِ

«Masiku bora zaidi ya dunia ni masiku kumi (ya mwanzo ya mwezi wa Mfungo tatu)»

صحيح الجامع ١١٣٣

Na wema waliopita walikuwa wakijipinda katika ibada pindi yaingiapo masiku haya kumi ya mwanzo ya mwezi wa Mfungo tatu, mfano huyu Said bin Jubair -Allah amrahamu ambaye ndiye mpokezi wa hadithi inayozungumzia ubora wa masiku haya kutoka kwa ibn Abbas -Allah amridhie- yeye alikuwa hivi:

كان سعيدُ بنُ جُبَيرٍ إذا دخل أيامُ العشرِ اجتهد اجتهادًا شديدًا ، حتى ما يكادُ يقدرُ عليه.

“Alikuwa Said bin Jubair pindi yaingiapo masiku kumi (ya mwanzo ya Mfungo tatu) hufanya juhudi kubwa (ya ibada) mpaka anakaribia kushindwa”

رواه الدارمي .

Tujitahidi kufanya ibada mbalimbali katika masiku haya na haswa kukisoma kitabu cha Allah , na kuchinja udh’hiyah.

        
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo pili 29, 1445H ≈ Jun/6, 2024M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz

         •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *