MASIKU YA TASHRIIQ /KUKAUSHA NYAMA

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net

قال رسول الله صلى الله عليه وسلم:

Amesema mjumbe wa Allah – swala na salamu za Allah ziwe juu yake:

” لا تصوموا هذه الأيام، فإنها أيام أكل وشرب وذكر لله عز وجل “

” Msifunge masiku haya, bila shaka masiku hayo ni masiku ya kula na kunywa na kumtaja Allah – aliyeshinda na aliyetukuka “

📚 رواه أحمد (10286) وصححه الألباني في السلسلة الصحيحة (3573).

[ Ameipokea Ahmad (10286) na ameisahihisha Al-baaniy katika silsilatu sswahiiha (3573) ]

‏قال ابن رجب – رحمه الله:

Amesema Ibn Rajab – Allah amrahamu –

‏فأيام التشريق يجتمع فيها للمؤمنين نعيم أبدانهم،بالأكل والشرب ونعيم قلوبهم بالذكر والشكر .

Basi masiku ya kukausha (nyama) kunakusanyika ndani yake kwa waumini neema za viwiliwili vyao,

kwa kula na kunywa na neema za nyoyo zao kwa kumtaja Allah na kumshukuru.

‏📚لطائف المعارف (٢٩١/١)

[ Latwaaifu l-ma’aarif (1/291) ]

‏قال النووي – رحمه الله

Amesema Annawawiy – Allah amrahamu –

ويستحب الإكثار في أيام التشريق من الأذكار، وأفضلها قراءة القرآن .

Inapendeza kukithirisha katika masiku (haya) ya tashriq kukithirisha nyiradi,
na bora ya (nyiradi) ni kusoma Qur’ani.

📚 الأذكار (٣٣٩)

[ Al-adhkaar (339) ]

Maelezo kutoka kwa mfasiri – Allah amuhifadhi

Masiku ya kusambaza nyama na kuzikausha (tashriq) nazo ni siku tatu zinazofuata baada ya sikukuu ya kuchinja yaani tarehe 11,12,13 .

Hizi ni siku ambazo kuna neema kubwa kwa waislamu, ni siku za watu kula na kunywa, pia ni masiku ya kuneemeka viwiliwili na miili ya waislamu na ni siku za kumtaja Allah.

Na ni haramu kufunga masiku haya ila kwa haji mutamatti’i au qaarin aliyekosa mnyama wa kuchinja yeye anaruhusiwa kufunga kwa baadhi ya wanachuoni .

Tanbihi: Yameitwa masiku ya kukausha nyama kwa sababu zamani walikuwa wakizisambaza nyama na kuzikausha ili zihifadhike , ama katika zama hizi Allah -aliyetukuka- ametupa neema ya mafriza watu hawana haja ya kukausha nyama , lakini ubora wa haya masiku na ibada zilizomo ndani yake zinabakia vile vile .

الله أكبر الله أكبر لا إله إلا الله والله أكبر، الله أكبر ولله الحمد.

Takbirah hizi mwisho wake ni baada ya swala ya alasir tarehe 13.

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Dhul-hijjah 10, 1442H ≈ Jul 20, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *