قال ابن القيم – رحمه الله – :
Amesema ibn l-Qayyim- Allah amrahamu-:
” إن أفضل العبادة العمل على مرضاة الرب في كل وقت بما هو مقتضى ذلك الوقت ووظيفته.
Hakika bora zaidi ya ibada ni kulifanya lile litakalomridhisha Mola mlezi,
katika kila wakati (kulifanya) lile linalotakiwa wakati (huo) ambao ni wakati wake (wa kulifanya) .
• فالأفضل في أوقات الأذان الاشتغال بإجابة المؤذن،
Basi lililo bora zaidi katika wakati wa adhana ni kushughulika na kumjibu muadhini,
وفي أوقات الصلوات الخمس الذهاب إلى المسجد، والصلاة في أول الوقت،
Na (lililo bora zaidi) nyakati
za swala tano ni kwenda msikitini na kuswali wakati wa mwanzo,
وفي وقت مرض أخيك المسلم عيادته،
Na (lililo bora zaidi) wakati ndugu yako muislamu anapougua ni kumtembelea (kumjulia hali),
وفي موته الصلاة عليه،
Na (lililo bora zaidi) pindi anapofariki ni kumswalia,
وفي وقت حضور الضيف القيام بواجب ضيافته .
Na (lililo bora zaidi) wakati anapohudhuria mgeni ni kusimamia takrima yake (mgeni).
📚 مدارج السالكين ( ١/ ١.٦)
Maelezo ya mfasiri:
Anasema ibn l-Qayyim- Allah amrahamu- kuwa ibada iliyokuwa bora zaidi ni mtu kutenda amali ya kumridhisha Allah katika muda ambao sheria imeeleza kuwa hiyo ibada ifanywe muda huo kwa maana kuifanya ibada katika wakati wake ,kisha akatoa mifano ya hilo:
1- Pindi muislamu anaposikia muadhini akiadhini basi bila shaka ibada bora zaidi muda huo kwake ni kumjibu yule muadhini kwa kuyasema yale anayoyasema muadhini kama alivyosema Mtume-swala na salamu za Allah zimfikie-:
” إِذَا سَمِعْتُمُ الْمُؤَذِّنَ فَقُولُوا مِثْلَ مَا يَقُولُ، …“
“Pindi munapomsikia muadhini basi semeni kama anavyosema muadhini ”
رواه مسلم
2- Pindi unapoingia wakati miongoni mwa wakati wa swala tano ,ibada bora zaidi muda huo ni kuacha kila kitu na kwenda kuswali kwa jamaa kama alivyosema Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie-:
” أفضلُ الأعمالِ الصَّلاةُ لوقتِها …“
“ Ibada bora zaidi ni kuswali katika wakati wake ”
صحيح الجامع
3- Pindi ndugu yako muislamu anapougua basi ibada bora zaidi muda huo ni kwenda kumtembelea na kumjulia hali, na hilo ni katika zile haki sita za muislamu kwa ndugu yake muislamu :
” .. وإذا مرض فعده، …“
Na pindi anapougua basi mtembelee
رواه مسلم
4- Pindi anapofariki ndugu yako muislamu ibada bora zaidi muda huo ni kuhudhuria jeneza lake kwa ajili ya kumswalia na kumuombea dua ،nalo pia ni miongoni mwa haki sita kama alivyosema Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie-:
وإذا مات فاتبعه.
“ Na pindi atapofariki basi fuata (jeneza lake) ”
رواه مسلم
5- Pindi unapofikiwa na mgeni basi ibada bora zaidi kwako ni kumfanyia takrima huyu mgeni kama vile kumuandalia chakula kizuri n.k hata kwa kujikalifisha katika kumfanyia takrima kwa maana ile siku ya kwanza aliyowasili kwako.
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo nne 30, 1443H ≈ Aug 28, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•