قال ابن الجوزي رحمه الله :
Amesema ibn l-Jauziy- Allah amrahamu-:
” والله لا يبقى في القيامة إلا الإخلاص ،
Naapa kwa Allah hakutobakia (siku) ya kiama isipokuwa matendo yaliyofanywa kwa ajili ya Allah.
وقبل القيامة لا يبقى إلا ذكر المخلصين ،
Na kabla ya (siku ya) kiama hakutobakia isipokuwa utajo wa wale waliofanya matendo yao kwa ajili ya Allah.
كم قول معروف مِن عالم ٍ لا يُعرَف قبره “
Ni maneno mangapi mazuri ya mwanawachuoni lisilojulikana kaburi lake .
📚 الآداب الشرعية لابن مفلح ( 244:2 )
Maelezo ya mfasiri:
Bila shaka miongoni mwa sharti za kukubaliwa matendo, ni kufanywa kwa ajili ya Allah ,ama matendo yaliyofanywa kwa ajili ya asiyekuwa Allah hayatokuwa na thawabu mbele ya Allah siku ya kiama , na pia matendo yaliyofanywa kwa ajili ya Allah matunda yake hubakia duniani hata baada ya kufariki mtendaji kama alivyosema imamu Malik-Allah amrahamu-:
ما كان لله دام واتصل، وما كان لغير الله انقطع وانفصل!
“ Lile lililokuwa kwa ajili ya Allah hudumu na huungana , na lile lililokuwa si kwa ajili ya Allah hukatika na hujitenga”
Na maneno haya aliyazungumza imam Malik-Allah amrahamu- baada ya kutunga kitabu chake cha hadithi
kinachoitwa “Al-muwattwa” na watu wengine nao wakatunga vitabu vilivyobeba jina hilo la “Al-muwattwa” , na watu walipomueleza imamu Malik-Allah amrahamu- yeye akazungumza maneno hayo tuliyoyataja hapo juu ,na kweli yalitokea yale aliyoyazungumza imamu Malik-Allah amrahamu- kitabu chake kimebakia mpaka leo watu wanakisoma na wanawachuoni wanakifundisha, na vile vitabu vingine vilivyobeba jina la “Muwattwa” vyote vimepotea na havijulikani !.
Tanbih:
Kama kisa hiki kikithibiti basi tunasema kuwa kufanya matendo kwa ajili ya Allah kuna matunda atakayoyapata mfanyaji hapa duniani kabla ya akhera kama vile kutajwa vizuri na kuombewa dua, na kubakia manufaa ya kile alichokifanya kwa ajili ya Allah, lakini pia hatusemi kuwa wale wale wanavyuoni wengine ambao walitunga vitabu vyenye jina hilo kuwa hawakutunga kwa ajili ya Allah ,bali tunasema kuwa Allah ameweka taufiki katika kitabu cha imamu Malik-Allah amrahamu- kikawa kinasomwa na kufundishwa mpaka leo .
•┈┈┈┈••✦✿✦••┈
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa : Mfungo mosi 7 , 1445H =Apr 15, 2024M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•