Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net
🔴 معنى قولهِ – صلَّى اللّٰهُ عَليهِ وسلَّمَ :-
Maana ya kauli yake- swala na salamu za Allah zimfikie-:
وما تَواضَعَ أحَدٌ لِلَّهِ إلَّا رَفَعَهُ اللَّهُ
“Na hakuna yeyote aliyenyenyekea kwa ajili ya Allah isipokuwa Allah humnyanyua”
قَالَ الشيخ ابن عثيمين- رحمه الله-:
Amesema sheikh ibn Uthaimin-Allah amrahamu-:
• تشمل من تواضع للخلق من أجل الله، كأن يتواضع الإنسان للفقير من أجل الله، أو يتواضع لأبيه وأمه من أجل الله، أو يتواضع لأخيه الكبير من أجل الله.
(Maneno haya) yanakusanya yule aliyewanyenyekea viumbe kwa ajili ya (kutaka radhi za) Allah,kama vile mtu akamnyenyekea fakiri kwa ajili ya kutaka (radhi za) Allah,au akamnyenyekea baba yake na mama yake kwa ajili ya kutaka (radhi za) Allah ,au akamnyenyekea kaka yake mkubwa kwa ajili ya kutaka (radhi za) Allah .
• وكذلك من تواضع لشرع الله، بحيث إذا سمع الله يأمر يقول: سمعا وطاعة وإذا سمع الله يخبر يقول: قبولا وتصديقا؛ لأن الخبر يقابل بالتصديق، والأمر يقابل بالامتثال.
vile vile yule aliyeinyenyekea sheria ya Allah kwa upande ambao akimsikia Allah anaamrisha husema: Nimesikia na nimetii ,na pindi anapomsikia Allah anaelezea habari (fulani) husema: Nakubali na nasadikisha, kwa sababu habari (za Allah) huelekewa kwa kusadikishwa ,na amri (zake) huelekewa kwa kutekelezwa.
• ومن التواضع لله مسألة ثقيلة على النفوس، إذا قال الإنسان قولا ثم عارضه آخر، وتبين الحق مع الآخر؛
Na katika kunyenyekea kwa ajili ya kutaka (radhi za) , Allah (kuna) masuala mazito katika nafsi (nayo ni haya) :
Ni pindi mtu ataposema kauli kisha mwingine akampinga, na haki ikabainika na (huyo) mwingine , (aliyepinga)
فإن كثيرا من الناس يصعب عليه أن يرجع عن قوله ولو بان الحق في خلافه، فهذا غير متواضع.
basi hakika wengi katika watu huwa ni uzito juu yao kuiacha kauli yake hata kama haki itadhihiri kinyume na hiyo (kauli) yake, basi (mtu) huyu si mnyenyekevu
• فيجب عليك أن تتواضع لله، وإذا تبين لك أن قولك خطأ، أن تضرب به عرض الحائط وتأخذ بالصواب،
Basi ni wajibu juu yako unyenyekee kwa ajili ya Allah ,na pindi inapobainika kwako kuwa kauli yako ni kosa (unatakiwa) kauli yako uipige ukutani na uichukue (kauli) ya sawa .
ولا تظن أن هذا يضعك عند الناس، بل هذا مما يرفعك عند الناس.
Na wala usidhani kuwa hili litakuweka chini/litakushusha mbele ya (macho ya) watu bali hili ni katika yale ambayo yanakunyanyua mbele ya watu .
📚 شرح عمدة الأحكام لابن عثيمين (٢\٢٦٢).
Maelezo ya mtarjumu:
Mwenye kunyenyekea kwa ajili ya kutafuta radhi za Allah ,yaani akaishusha nafsi yake kwa ajili ya kutafuta radhi za Allah na wala si kwa ajili ya chochote katika duniani ,malipo ya mtu huyu ni kunyanyuliwa na Allah kidaraja ima duniani au akherah au sehemu zote mbili yaani duniani na akhera, na unyenyekevu umegawanyika sehemu mbili -kama alivyoeleza sheikh :
1- Kunyenyekea maamrisho ya Allah mfano : Kutekeleza ibada ya swala ,kutoa zaka, kumtii Allah na Mtume wake- swala na salamu za Allah zimfikie-.
2- Kuwanyenyekea waja wa Allah kwa ajili ya kutaka radhi za Allah mfano: Kumsalimia fakiri asiyejiweza, kutokuwa na kiburi ,na mtu yeyote ambaye anatabia ya unyenyekevu basi watu humpenda na kinyume chake ni yule mwenye kiburi na kujiona mtu huyu Allah watu humchukia na hawampendi na humdharau .
Mtarjumu: Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo sita 22, 1443H ≈ October 28, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•