MAUTI

كتب الشيخ صالح العصيمي -حفظه الله تعالى- عبر حسابه على تويتر .

Ameandika sheikh Swaleh Al-Uswaim -Allah amuhifadhi- kupitia ukurasa wake wa twitter (maneno yafuatayo) :

هجرك ذكر الموت، وكراهيتك ذلك لا يجعلك بعيدًا عنه، فلكلِّ نفسٍ أجلٌ محتومٌ، اللَّهمَّ أحسن خاتمتنا.

Kuacha kwako kukikumbuka kifo, na kukichukia kwako hicho (kifo), hakikufanyi kuwa mbali nacho ,kila nafsi ina muda (usioepukika), ewe Allah ufanye mwisho wetu kuwa ni mwema .

الأربعاء ٢ ربيع الأول ١٤٤٤ه‍

Maelezo ya mfasiri:

Kifo ni jambo la lazima kwa kila mmoja sawasawa ukikumbuke au usikikumbuke kwa maana hata kama haupendi kuambiwa habari za kifo na unachukia kusikia habari zake lakini ipo siku kitakufika ,na kama ukilijua hili basi yafanyie kazi maneno ya Mtume-swala na salamu za Allah zimfikie- pale aliposema :

” أكثِرُوا ذكرَ هادِمِ اللذَّاتِ “ . يعني : الموتَ

“ Kithirisheni kukikumbuka chenye kukata ladha”.

Anakusudia kifo .

Ufafanuzi :

Bila shaka kukumbuka kifo ni sababu ya kuondoa mapenzi ya dunia katika moyo na kuzidisha ibada imbazo zitamnufaisha muislamu baada ya kifo, ama yule mwenye kukikumbuka kifo ukumbukaji wenye kumpelekea akawa na majonzi na mawazo ya kuwa ataachana na vipenzi vyake katika hii dunia na akaishia na hayo majonzi na huzuni tu bila shaka ukumbukaji huu hautomnufaisha .

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo sita 27, 1444H ≈ Oct 23, 2022M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *