MAZINGATIO KATIKA KISA CHA NABII YUSUF- AMANI IWE JUU YAKE -06

https://t.me/fawaidussalafiyatz

.

Makala namba (6) :

قال تعالى :

Amesema (Allah) aliyetukuka-:

اقْتُلُواْ يُوسُفَ أَوِ اطْرَحُوهُ أَرْضًا يَخْلُ لَكُمْ وَجْهُ أَبِيكُمْ وَتَكُونُواْ مِن بَعْدِهِ قَوْمًا صَالِحِينَ

9 ” (Wakasema) Muueni Yusuf ,au mtupeni katika ardhi (isiyojulikana) ili uso wa baba yenu ukuelekeeni nyinyi peke yenu (kwa sababu ya kutokuwepo kipenzi chake) ,na baada ya haya mtakuwa watu wema (mtatubia kwa Allah) “

Maelezo:

Ndugu wa Yusuf walipanga njama na mipango ya kumpoteza ndugu yao Yusuf- Amani iwe juu yake- wakasema wamue au wampoteze mbali ,lengo lao ni kuwa asiwepo na asionekane kwa baba yao ,na wakifanya hivyo basi baba yao atawapenda kwa sababu yule kipenzi chake atakuwa hayupo .
Na wakapeana moyo wa kufanya ubaya huo ,kwa kuambiana kuwa baada ya uovu huo wataleta toba kwa Allah -aliyetukuka- na watakuwa watu wema ,au baada ya kumuua au kumpoteza Yusuf -amani imfikie- wataishi maisha mazuri na hali yao itakuwa nzuri kwa sababu baba yao atawapenda zaidi na mapenzi ya baba yao yatabakia kwao pekee .

Tunaona kuwa nafsi ikiingiwa na husuda na mafundo huwenda ikaona kuwa dhambi kubwa kuwa ni ndogo kwa sababu ya chuki iliyopo katika nafsi kama walivyofanya ndugu wa Yusuf -amani imfikie- ,pindi walipotaja kosa la kuua na wakatanguliza toba, na pia ndani ya tukio hili tunaona kuwa Allah anakubali toba ya dhambi ya kuua kwa sababu Allah -aliyetukuka- pindi alipotaja njama zao za kuua na kutanguliza toba kabla ya hapo hajawapinga ikawa ni ishara kuwa toba ya muuaji inakubaliwa .

Muandaaji: fawaidusalafiya.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiya.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Ramadhani 19, 1442H ≈ May 1, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *